Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakijipongeza na medali zao baada ya kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango wa matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo mapema hii leo. Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ili kuunga mkono jitihada hizo