Ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Wednesday November 25 2020
kujinyonga pic
By Mary Clemence

Katavi. Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka na maiti yake kukutwa juu ya mwembe mtaa wa Mnazi mmoja manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Akizungumza na Mwananchi Digital mjumbe wa mtaa huo, Juma Gogomoka amesema alipata taarifa za tukio hilo saa 1:45 kutoka kwa mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Amesema mtu huyo alimueleza kuwa akiwa shambani kwake alipewa habari  na wanawake waliokwenda kuchuma maembe kuwa kuna mwili wa mtu unaning’inia kwenye mti.

"Baada ya kuambiwa nilifika eneo hilo na kushuhudia mwili lakini sikuutambua kwa kuwa hakuwa mkazi wa mtaa wangu. Nilitoa taarifa polisi walifika tukauchukua  na kuupeleka hospitali.”

“Eneo la tukio nilikuta mfuko wa plastiki na baada ya polisi kufika walipekua tulibaini kuwa ndani yake kulikuwa na suruali  mbili na shati na baadaye hospitali walipekua wakaona karatasi iliyoandikwa namba za simu wakapiga ikapokelewa na nesi aliyedai kuwa marehemu atakuwa alifika kwenye hospitali hiyo, kupewa namba ni kiashiria cha ushauri kuhusu huduma kutokana na hali aliyokuwa nayo kiafya," alisema mjumbe huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi,  Benjamini Kuzaga amethibitisha kutokea tukio na kwamba limeripotiwa Novemba 23, 2020 na mjumbe wa serikali ya mtaa.

Advertisement

"Polisi walifika eneo la tukio umbali wa mita 300 kutoka kwenye makazi ya watu ni kweli alikuwa na kadi ya matibabu ya afya, tunaendelea kufuatilia taarifa zake ili atambuliwe na ndugu zake," amesema Kuzaga.


Advertisement