Akutwa amefariki eneo la Jangwani Dar

Monday September 20 2021
Auawa pc
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina mara moja amekuwa akiwa amefariki katika eneo la Jangwani pembezoni mwa kituo cha mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, leo Septemba 20, 2021.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Debora Magiligimba amekiri kufahamu tukio hilo alipopigiwa simu.


Mwandishi wa habari hizi alikuwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, ambapo baadhi ya watu waliokusanyika kumwangalia mtu huyo, ambapo mmoja wa dereva bodaboda aliyejitambulisja kwa jina moja la Kamugisha amesema bila shaka huyo alikuwa dereva mwenzao.


“Tumekuwa tukishuhudia madereva wa bodaboda wakivamiwa na kuporwa pikipiki zao. Kuna vijana wanakusimamisha kama wateja, ukisimama wanakuvamia na kupora pikipiki nan a ukishana nao wanaweza kukua,” anasema.


Naye dereva bodaboda Ramadhani Said maarufu kwa jina la Mtu Pesa mkazi wa Kigamboni alisema inawezekana mwenzao ameuliwa na majambazi.


“Kwa kweli kipindi hiki kimekua kigumu sana kiusalama, kwani eneo la Jangwani limekuwa na matukio ya uvamizi kwa waendesha pikipiki na magari. Tunaomba jeshi la Polisi lifanye doria usiku na mchana ili kuwabaini wahalifu eneo hili,” amesema Ramadhani.

Advertisement
Advertisement