Akzo Nobel N.V yaihodhi Kansai Paint Co. Ltd

Thursday June 16 2022
tangapic

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kansai Plasco East Africa, Arvind Shekhawat

By Maliki Muunguja

Kansai Paint Co. Ltd, wazalishaji wa bidhaa ya “Kansai Paint” wameingia makubaliano ya kuuza kampuni yake tanzu iliyoko barani Afrika kwa kampuni ya Akzo Nobel N.V. Akzo Nobel N.V ni kampuni kubwa ya uuzaji wa rangi duniani.

Mauzo yake yametokana na kukamilika kwa taratibu zote stahiki kutoka katika mamlaka husika na malipo yake yatakamilika mwanzoni mwa mwaka 2023. Kunishi Moro, ambaye ni Rais wa Kansai Paint, anasema kuwa, “Tumejiridhisha kuwa kampuni ya Akzo Nobel ni kampuni kubwa ya rangi na kwa kuwa bidhaa hiyo ndiyo mhimili wa uendeshaji wa kampuni, tunaamini kupitia bidhaa hiyo itaweza kufungua fursa nyingi za biashara na baadaye kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi za Kiafrika.”

Kampuni hiyo imejijengea historia ya aina yake tangu mwaka 1646 na imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Euronext Amsterdam. Pia inaelezwa kuwa kampuni inaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 150, ikiajiri watu takriban 33,000 duniani na kufanya mauzo yanayokadiriwa kufikia Euro 9.6 bilioni (sawa na Yen 1.3 trilioni) mwaka 2021.

Kufuatia mkakati wake wa “Kukuza na Kuuza” kampuni hiyo imekuwa ikisambaza bidhaa mbalimbali za rangi kwa nchi za Afrika Kusini na Kenya nk. Wawekezaji hao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika ustawi endelevu wa nchi nyingi za Kiafrika kwa muda mrefu kupitia miradi yake mbalimbali ya maendeleo na bidhaa endelevu sambamba na urudushaji kwa jamii, taasisi ya SOS Children ikiwa mojawapo ya jamii hizo.

 “Kuhodhi shughuli za kampuni ya Kansai Paint barani Afrika kutatuwezesha kutanua wigo wetu wa biashara ya bidhaa mbalimbali za rangi barani humo na kutuhakikishia fursa ya ukuaji zaidi. Ununuzi wa kampuni hiyo unatafsiri jitihada za dhati za uvumbuzi na uendelevu wa kampuni hiyo na tuna shauku ya kuchanganya ujuzi wetu, ambao utachagiza kuwa na bidhaa bunifu na masuluhisho endelevu kwa wateja wetu,” anaeleza Thierry Vanlacker, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Akzo Nobel.

 Kwa kampuni za Kansai Plascon Afrika hususan zile zilizoko katika nchi za Kenya, Tanzania, Uganda, Zanzibar na Burundi makubaliano haya ni fursa ya ukuaji zaidi. "Tumekuwa na mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Kansai Paint na kuweza kukabiliana na kutokutabirika kwa soko wakati wa janga la Uviko-19.

Advertisement

Tunashukuru kwa msaada wa dhati wa kampuni ya Kansai Paint. Kuelekea mbele, tunaamini kuwa kampuni ya Akzo Nobel itazipeleka biashara zetu mbali zaidi na kwa kuwa kampuni hiyo inajielekeza katika uwekezaji kwenye usalama, jamii na utawala (ESG) ambapo inajikita katika uvumbuzi, maendeleo ya wafanyakazi, fursa pana za kada hiyo vile vile mafanikio ya muda mrefu ya biashara yake barani Afrika,” anasema Arvind Shekhawat, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kansai Plascon East Africa.

Plascon ina uongozi mkubwa wa soko kwa Uganda na ikiwa kiongozi katika Ukanda wa Afrika Mashariki, katika nafasi hiyo, ina fursa kubwa ya kukuza biashara yake kuipeleka katika hadhi ya juu zaidi chini ya uongozi mpya wa Akzo Nobel.

Safari ijayo kulingana na Ofisa huyo itakuwa ni aina yake kwa kuwa kampuni imejipanga kutengeneza mkakati, bidhaa, huduma na chapa zitakazoongeza thamani zaidi katika soko la Afrika Mashariki kwa namna na utaratibu endelevu.

Akizungumzia jambo hilo, Jan-Piet Van Kesteren, Mtendaji Mkuu wa Akzo Nobel barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika anasema kuwa, “Hatua ya kuhodhi kampuni ya Kansai Paint Africa una faida kubwa katika biashara yetu iliyojiimarisha ikiendeshwa katika nchi tisa barani Afrika.

Pia hatua hiyo inakwenda kuliimarisha jalada letu la nafasi za uongozi katika masoko yanayovutia na chapa za hadhi ya juu barani Afrika, huku ikichochea ukuaji wa biashara zaidi katika masoko yanayokua kwa kazi.

Advertisement