Asilimia 85 waliofanya mtihani kidato cha nne 2020 wamefaulu

Asilimia 85 waliofanya mtihani kidato cha nne 2020 wamefaulu

Muktasari:

  • Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yakionyesha kuwa asilimia 85 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yakionyesha kuwa asilimia 85 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Kwa mujibu wa Necta iliyotangaza matokeo hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 kupitia kwa katibu mtendaji wake, Dk Charles Msonde, watahiniwa 434,654 walifanya mtihani huo na 373, 958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali.

Dk Msonde amesema kwa matokeo hayo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 5.19.

Matokeo ya kidato cha nne 2020/2021 haya hapa

Katika mtihani huo Paul Luziga wa sekondari ya Pandahill iliyoko Mbeya amekuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa.