Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki ajalini

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy

Muktasari:

Balozi huyo amefariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Tanga. Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushi amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Mushi aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

 Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Desemba 15, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

"Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia," amesema Balozi Sokoine.