Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bawacha: Wanaopinga Katiba Mpya hawakupingi, bali wanakupima

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Catherine Ruge

Moshi. Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Catherine Ruge amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuandika historia itakayosomwa na vizazi vyote kwa kuwezesha upatikanaji wa Katiba mpya.

Ruge ametoa kauli hiyo leo Machi 8, 2023 wakati akitoa taarifa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia yaliyoandaliwa na baraza hilo ambayo yanafanyika kitaifa Ukumbi wa Kuringe mjini Moshi na mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema wanafahamu jitihada zinazofanywa na Rais pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe za kuhakikisha inapatikana Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya mwaka 2025. lakini kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wakimkatisha tamaa.

"Tunafahamu unafanya jitihada kubwa na Mwenyekiti Mbowe kuhakikisha tunapata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2025, usiogope hujuma za wanaotaka ushindwe kama wao walivyoshindwa huko nyuma," amesema.

"Ukichunguza vizuri mheshimiwa Rais hata hao wanaopinga jitihada zako za kupata katiba mpya hawakupingi bali wana kupima. Ni wakati wako Rais kuandika historia ambayo itasomwa vizazi vijavyo," amesema.

"Tunafahamu pamoja na jitihada zako za kujenga Taifa salama na lenye utengamano. Wapo wengi ambao wanajaribu kukukatisha tamaa, si jambo la bahati mbaya kwamba wanaojaribu kukukatisha tamaa  ni wanaume, Bawacha tunakwambia usiogope," amesema.

Ruge amesema Rais yupo mahali sahihi, pamoja na kwamba ana chama chake kwa kuwa ana nafasi ya kusikiliza na kutekeleza vilio vya kina mama nchini kote.
Amesema hadhi ya kina mama na watoto wa Taifa hili havifanani na mchango wanaoutoa, kwa kuwa wanawake wanaishi maisha duni, na kwamba hawana uhakika kama Rais analitambua hilo.
"Wanawake hawa wanawakilisha wanawake milioni 31 nchi nzima kwani Bawacha ni sauti ya kina mama wote Tanzania  ikiwemo wewe," amesema.

"Rais unapokuwa kule kwenye chama chako wanawake wenzetu wa CCM hawakwambii ukweli wanakwambia mambo unayopenda kusikia kama mama unaupiga mwingi hata mahali ambapo walistahili kukueleza changamoto za kina mama ili uweze kuzitatua," amesema.

"Bawacha tunaamini pamoja na mazuri unayoyafanya utafungua sikio lao ili kusikia changamoto za kina mama na yale ambayo yanahitaji utashi w