Bayern kucheza na Al Ahly au Al Duhail klabu bingwa ya dunia Qatar

Muktasari:

  • Bayern Munich itacheza na ama mabingwa wa soka wa Afrika, Al Ahly au Al Duhail ya Qatar katika nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia Februari 2021 baada ya ratiba kupangwa jana Jumanne Januari 19, 2021 jijini Zurich.

Zurich, Uswisi (AFP). Bayern Munich itacheza na ama mabingwa wa soka wa Afrika, Al Ahly au Al Duhail ya Qatar katika nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia Februari 2021 baada ya ratiba kupangwa jana Jumanne Januari 19, 2021 jijini Zurich.

Mechi hiyo ya nusu fainali itachezwa Jumatatu Februari 8, 2021  kwenye Uwanja wa Ahmad Bin Ali mjini Al Rayyan, nje kidogo ya Jiji la Doha.

Kabla ya hapo, Al Ahly na Al Duhail zitakutana Februari 4, 2021 katika uwanja ulio karibu wa Education City, sehemu nyingine itakayotumika kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Al Ahly, vigogo wa Cairo wanaofundishwa na Pitso Mosimane wa Afrika ya Kusini, ndio klabu yenye mafanikio kuliko zote barani Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika mara tisa.

Wakati huohuo Al Duhail, ambayo kocha wake ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu za Rennes na Nottingham Forest, Sabri Lamouchi, imeingia katika michuano hiyo ikiwa mwenyeji.

Katika mechi nyingine, klabu ya Mexico ya UANL, mabingwa wa Amerika Kusini, watakutana na mabingwa wa Asia, Ulsan Hyundai ya Korea Kusini Februari 4 katika nusu fainali ya kwanza itakayochezwa Februari 7.

Klabu za Brazil, Santos na Palmeiras zitavaana katika mechi baina ya timu hizo za Amerika Kusini itakayochezwa uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro Januari 30.

Timu nyingine ya Brazil, Flamengo ilifungwa mwaka 2019 na Liverpool, huku klabu za Ulaya zikitwaa ubingwa huo kwa miaka saba iliyopita.

Zilianza kwa Bayern kutwaa ubingwa huo nchini Morocco