Benki ya UBA yaingia ukanda wa EMEA, yazindua tawi la UBA DFIC, Dubai

Wednesday July 20 2022
New Content Item (1)

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji, Hazina na Huduma za Benki za Kimataifa wa UBA, Ndubisi Chiugo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC), Prince Arif Amiri, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu, Gavana wa Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC), Essa Kazim, Mkurugenzi Mkuu /Mtendaji wa UBA Group, Kennedy Uzoka na Mkurugenzi Mtendaji wa UBA (DIFC), Vikrant Bhansal katika uzinduzi rasmi tawi la Benki ya UBA (DIFC) huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), siku ya Alhamisi.

Benki ya UBA, benki ya kima-taifa ya Afrika imekuwa ikifanya kazi kwa zaidi ya miongo saba iliyopita. Leo, benki hii ipo katika nchi 20 za Afrika, Uingereza, Marekani na Ufaransa.

Benki hiyo imepanua shughuli zake na kugonga hodi hadi Umo-ja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuzindua rasmi tawi lake jipya katika Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC).

Tawi la DIFC litafanya kazi chini ya leseni ya Kundi la 4 na itasimamiwa na Mamlaka ya Huduma za Kifedha ya Dubai (DFSA), Wakala wa Usimamizi wa Fedha wa Ukanda Maalum wa Kiuchumi, Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai.

Tawi la UBA (DIFC) litahudumia mashirika na taasisi za kifedha na wateja kote Mashariki ya Kati likilenga zaidi huduma za benki kwa nchi nyingine duniani, usimamizi wa uhusiano na huduma za ushauri.

Kupitia upanuzi huu mpya, Benki ya UBA itaweza kutumia fursa za maeneo ya Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Kusini (MEASA), ambayo inajumuisha nchi 72 zenye takriban watu bilioni 3 na Pato la Taifa la Dola za Marekani trilioni 7.7 na hivyo, kuimarisha umiliki wake mkubwa kama Benki ya Dunia ya Afrika, kuwezesha biashara na mtiririko wa mtaji kati ya Afrika na dunia nzima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni mshirika mpya huko Dubai siku ya Alhamisi, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu, anaeleza kuwa pamoja na benki hiyo kuingia katika ukanda wa Ghuba, inaendelea kuzingatia nia yake ya kimkakati ya kuwa kiongozi wa soko linapokuja suala la kufanya biashara barani Afrika.

Advertisement

Anasema kuwa,”Kushirikiana na matawi yetu katika nchi 20 za Afrika na vituo vikuu vya fedha vya London, New York na Paris, UBA (Tawi la DIFC), kutawezesha ufanyikaji shughuli za biashara kati ya Mashariki ya Kati na Afrika lakini pia itawezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya biashara na uwekezaji,” anasema Elumelu.

“Tumeisubiria siku hii kwa muda mrefu kwani ni mara ya kwanza kuiingiza biashara yetu katika sehemu hii ya dunia. Tunajua kwamba upanuzi wetu wa kimataifa haujakamilika ikiwa hakuna ofisi zetu katika ghuba hiyo,” anaendelea.

Mkurugenzi Muu/ Mtendaji wa UBA Group, Kennedy Uzoka, ambaye pia alizungumza kwenye hafla hiyo anasema,

“Leo, tuko rasmi katika mabara manne kote ulimwenguni, tufanya kazi katika nchi 24, tunahudumia zaidi ya wateja milioni 35 na bado tunaendelea kukua.

New Content Item (1)

Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC), Prince Arif Amiri, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu, Gavana wa Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC), Essa Kazim, Mkurugenzi Mkuu / Mtendaji wa UBA Group, Kennedy Uzoka na Mkurugenzi Mtendaji wa UBA (DIFC), Vikrant Bhansal katika uzinduzi rasmi wa tawi la Benki ya UBA (DIFC) huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), siku ya Alhamisi.

“Sisi ndio benki pekee yenye asili ya Nigeria ambayo imeenea kutoka Nigeria hadi UAE. Wale waliotutangulia wamepitia maeneo mengine na hiyo inaonyesha nguvu na heshima walizo nazo Mamlaka za Dubai kwa UBA. Uwepo wetu Dubai unathibitisha kwamba UBA ni benki yenye nguvu, inayopanua wigo wake kote ulimwenguni.Mamlaka na mazingira ya biashara hapa DIFC yanavutia na UBA inaiona Dubai kama lango la Afrika na ndiyo maana tuko hapa, kuwa karibu na wateja wetu, kushirikiana nao na kuwezesha biashara na mtiririko wa ufanyanyaji biashara kuingia Afrika kupitia kampuni washirika wa UBA. Kwa hiyo, tunafurahi sana,” anaeleza Uzoka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UBA (DFIC), Vikrant Bhansali anasema, “Biashara na Uwekezaji Afrika unapanuka katika kanda za Ghuba na Asia. Kutokana na uwepo wa Benki ya UBA katika vituo vya fedha vya kimataifa, UBA (DFIC) itaongeza uwezo wa benki kuwezesha upatikanaji wa wawekezaji wa Ghuba na benki kwenye masoko ya Afrika. Tutawezesha biashara na kusaidia kukuza uwekezaji barani Afrika katika sekta zote.”

“UBA (DFIC) inadhihirisha uhusiano mkubwa kati ya Dubai na Afrika. Ni mwanzo mzuri kwani tunatazamia kupata mwingiliano zaidi, kuelekeza biashara zaidi na uwekezaji barani Afrika, na kwa UBA DIFC, tunakaribia kufikia malengo yetu. DIFC itaendelea kutafuta ushirikiano ambao utachagiza uhusiano wenye faida kwa pande zote mbili kama tulivyo-shuhudia hivi punde na Benki ya UBA,” anafafanua Ofisa Mkuu Mtendaji wa Mamlaka ya Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha Dubai (DIFC), Arif Amiri wakati wa hafla ya kukata utepe.

Kuhusu UBA Group

Benki ya UBA ni taasisi ya fedha inayoongoza barani Afrika, inayotoa huduma za kibenki kwa zaidi ya wateja milioni 37 katika ofisi 1,000 za biashara na vituo vya huduma za fedha katika nchi 20 za Afrika.

Kwa uwepo wake New York, London na Paris na sasa UAE, UBA inaunganisha watu na biashara kote barani Afrika kupitia huduma za benki kwa wateja wa kawaida, biashara na kampuni, huduma za kutuma fedha nje ya nchi na fedha zito-kanazo na wateja wanaoishi nje ya nchi (diaspora) na huduma za benki za ziada.

Advertisement