Advertisement

Bocco atupia ‘hat trick’ Simba ikijipigia Coastal

Sunday November 22 2020
bocco pic

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco

By Mwandishi Wetu

Arusha/Dar. Mshambuliaji wa Simba, John Bocco jana alifunga mabao matatu ndani ya dakika 45 kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 7-0 ilioupata timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara.

Bocco aliandika rekodi hiyo walipokaribishwa na Coastal Union katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kwenye mchezo ulioonekana kuwa wa upande mmoja.

Hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika Simba ilikuwa ikiongoza mabao 5-0, ambapo Hasssan Dilunga aliitanguliza katika dakika ya saba akipokea pasi ya Bocco, kisha Bocco akafunga matatu mfululizo dakika za 25, 27 na 37 kabla ya Bernard Morrison kufunga la tano dakika ya nyongeza ya kipindi hicho.

Kwa mabao hayo matatu ya Bocco anakuwa mchezaji wa pili msimu huu kufunga ‘hat trick’, akimfuatia Adam Adam wa JKT Tanzania aliyefanya hivyo katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Mwadui FC.

Pia Bocco amefikisha mabao saba na kuwa kinara kwenye ligi akiwaacha Prince Dube wa Azam na Adam wenye mabao sita kila mmoja.

Simba ilipata bao la sita katika dakika ya 60 na la saba dakika ya 85 yaliyofungwa na Clatous Chama.

Advertisement

Nahodha wa Simba, Bocco aliwapongeza wachezaji wenzake kwa kujituma na kupata ushindi.

Naye nahodha wa Coastal Union, Salum Ally alisema walifanya makosa wakaadhibiwa.

Mechi zingine zilizochezwa jana; Azam FC ilifungwa bao 1-0 na KMC katika Uwanja wa Uhuru, huku Gwambina ikiifunga

Advertisement