Bunge la Tanzania labadili ratiba

Bunge la Tanzania labadili ratiba

Muktasari:

  • Bunge limebadili ratiba ya shughuli zake baada ya makubaliano ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dodoma. Bunge limebadili ratiba ya shughuli zake baada ya makubaliano ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Naibu Spika,  Dk Tulia Akson amesema kamati ya uongozi ya Bunge ilikutana na kuweka ratiba hiyo ambapo sasa hotuba ya Serikali itasomwa Juni 10, 2021.

Awali ratiba ilionyesha kuwa Waziri wa Fedha angesoma hotuba ya bajeti ya Serikali Juni 17, 2021 hivyo kwa ratiba mpya siku saba zimepunguzwa.

"Kwa hiyo naomba wabunge muangalie ratiba hiyo kwenye vishikwambi vyetu ambapo ratiba za uwasilishaji wa bajeti za wizara nazo zimebadilika," amesema Dk Tulia.

Kutokana na ratiba hiyo, ni wazi kuwa baadhi ya Wizara zitapunguzia muda wa siku zao za kujadili bajeti uliokuwepo awali.