Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM, Chadema wajitosa sakata la waandishi MCL kushambuliwa

Muktasari:

  • Vyama vya CCM, Chadema vimeungana na wadau wengine wakiwamo Serikali na asasi za kiraia kulaani tukio la kushambuliwa kwa wanahabari na dereva wote wa kampuni ya Mwananchi wakati wakitekeleza majukumu yao.

Dar es Salaam. Vyama vya CCM na Chadema, vimelaani tukio la kushambuliwa kwa wanahabari na dereva wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wakati wakitelekeleza majukumu yao katika uwanja wa Bulyaga, Temeke.

Tukio hilo lilitokea mchana wa Jumamosi, Julai 22, 2023 wakati waandishi na dereva walipofika kufuatilia maandalizi ya mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chadema uliofanyika jana Jumapili na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika.

Waandishi waliokumbwa kadhia hiyo ni Fotune Francis, Sunday George pamoja na dereva aliyekuwa akiwaendesha Omary Mhando. Katika tukio hilo, walishambuliwa, kujeruhiwa, kuporwa na kuharibu mali, vitendea kazi vya wanahabari hao.

Katika taarifa zao kwa vyombo vya habari walizozitoa leo Jumatatu Julai 24, 2023 vyama hivyo, vimeelezea kulaani na kukemea kitendo hicho ambacho cha uvunjifu wa amani huku wakiagiza dola kuwachukulia hatua waliohusika kuwashambulia.

“CCM ikiwa mdau mkubwa wa tasnia ya habari na vyombo vya habari, inatoa wito kwa jamii kutambua, kuheshimu na kulinda uhuru wa wanahabari.

“Wanahabari wana wajibu wa kuelimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusua maendeleo ya uchumi, kijamii na kisiasa,” amesema Sophia Mjema ambaye ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi.

Wakati CCM wakieleza hayo, Chadema pia kimeungana vyama vingine pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu kulaani tukio hilo, wakisema linaahatarisha amani na utulivu wa nchi.

“Tunavitaka vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria mara moja wote waliohusika ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa ya amani, utulivu na usalama,” amesema John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema.

Katika taarifa hiyo, Chadema ameongeza kuwa, “Kuumiza waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao kisheria ni jambo lisilovumilika kwasababu yoyote ile. Tunaendelea kufuatilia tukio hili ili kuona Serikali na vyombo vya dola watachukua hatua gani madhubuti,”amesema Mrema.