CCM yashinda ubunge Konde

Sunday July 18 2021
uchaguzi pc
By Jesse Mikofu

Pemba. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Yassin Khamis ametangaza Shekha Fakhi Mpemba kuwa mshindi wa jimbo hilo kwa kupata kura 1796.

Mpemba amewashinda wenzake 11 akifuatiwa na Mohamed Said Issa wa ACT Wazalendo aliyepata kura 1373.

Khamis amesema kura zilizopigwa ni 5050, kura halali ni 5020 na kura 30 zimekataliwa.Advertisement