Chadema yadai Mbowe kuugua akiwa kituoni

Monday July 26 2021
mbowe pc
By Fortune Francis

Dar es Salaam. Chama Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelitaka Jeshi la Polisi kumpeleka hospitali mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ili kupatiwa matibabu.

 
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Julai 26, 2021 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema imeeleza kuwa wamepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambao walimtembelea asubuhi katika kituo cha polisi Osterbay.


Hata hivyo Mwananchi Digital ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai ili kuzungumzi suala hilo amesema atafutwe baadaye.


Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa kiongozi huyo anaumwa na tayari wameshalijulisha Jeshi la Polisi kuhusu kuugua kwake, wakitaka apelekwe hospitali kwaajili ya vipimo na matibabu.


“Mpaka muda huu wa saa sita kamili mchana, polisi hawajampeleka hospitali kwaajili ya vipimo na matibabu,”imeeleza taarifa hiyo.


“Chama kimeelekeza mawakili wake kufika mara moja kituo cha Polisi Oysterbay kwaajili ya kumuona mwenyeiti huyo.”

Advertisement
Advertisement