Chadema yakusanya Sh234.6 milioni kuwatoa kina Mbowe

Wednesday March 11 2020
pic mchango

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimekusanya zaidi ya Sh234.6 milioni zilizochangwa na wanachama na wapenzi wa chama hicho kwa ajili ya kulipa faini ya Sh350 milioni walizotozwa viongozi wa chama hicho.
Viongozi hao wanane wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe walihukumiwa jana kulipa faini ua kutumikia kifungo cha miezi mitano jela baada ya kukutwa na hatia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Machi 11, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohammed amesema kati ya fedha hizo Sh176.94 milioni  zimechangwa kwa simu, Sh52.74 milioni zimechangwa kupitia benki na Sh 4.7 milioni zimechangwa kama fedha taslim.


"Tulipotangaza jana kuchangia, mwitikio umekuwa mkubwa. Kuna wengine wameuza kuku zao, mayai, nyama. Tumepata jumla Sh234,469,000," amesema Mohammad.
Amesema kati ya fedha hizo wametumia Sh100 milioni kulipa mahakamani na kupata code number ya washitakiwa.
"Mawakili wetu wapo tumepata remove order ya kuwatoa wabunge wanawake. Halima Mdee gharama yake Sh40 milioni, Esther Matiko Sh30 milioni na Esther Bulaya Sh30 million," amesema

Advertisement