Chongolo aendesha kikao cha kwanza baada ya kuteuliwa

Saturday May 01 2021
UTAMBULISHOPIC
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo jana  Ijumaa Aprili 30, 2021 muda mfupi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo aliripoti ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho wa wajumbe wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na ofisi yake inaeleza kuwa pamoja  na wajumbe wengine wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa (Nec), kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe wapya akiwemo naibu katibu mkuu, Christina Mndeme na katibu wa itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka.

UTAMBULISHOOOPICCC

Pia walikuwepo viongozi wastaafu wakiongozwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo na aliyekuwa katibu wa Nec oganaizesheni, Pereira Silima.


Advertisement