Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Maiga akabidhi misaada kwa waathirika wa moto Rombo

Muktasari:

Kaya Saba zilizokumbwa na ajali ya moto na kuteketeza vyumba 11 na mali zilizokuwemo ndani katika Kijiji cha Mbomai, kata ya Tarakea Motamburu, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro wameanza kupatiwa msaada wa vyakula na malazi.


  

Rombo. Kaya Saba zilizokumbwa na ajali ya moto na kuteketeza vyumba 11 na mali zilizokuwemo ndani katika Kijiji cha Mbomai, kata ya Tarakea Motamburu, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro wameanza kupatiwa msaada wa vyakula na malazi.

Moto huo ulitokea usiku wa Februari 6, 2023 na kuteketeza vyumba hivyo  11 vya wapangaji na kuunguza mali zilizokuwemo ndani kama vyakula, mavazi na fedha ambapo wananchi hao hawakuweza kuopoa chochote.

Akizungumza na familia hizo leo, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga wakati akikabidhi msaada wa vyakula na magodoro, ameziomba familia hizo kuwa na subira wakati serikali ikiangalia namna ya kuwafanyia utaratibu wa kupata makazi mapya.

"Leo tumekuja na hivi vitu vidogo, magodoro saba, magunia manne ya mahindi, sukari, mashuka, unga na sufuria maana tumeona hapa ndio pakuanzia ili kuhakikisha mnakaa katika hali ambayo ni nzuri kwa kipindi hiki kwanza," amesema.

"Kwa hiyo sisi tunaendelea na vikao lakini Serikali tumeshachukua hatua ili familia hizi ziweze kupata mahali pa kuishi, tumeshaongea na huyu mwenye nyumba na tutaharakisha ili nyumba hii iweze kurudi kama ilivyokuwa na sisi tuko nyuma yenu,"asema Kanali Maiga.

Wakizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, baadhi ya Waathirika hao wa moto, wamemshukuru Mkuu huyo wa wilaya kwa kuwapatia msaada wa vyakula na mavazi.

Mmoja wa waathirika wa ajali hiyo ya moto, Selina Frank ameishukuru ofisi ya Mkuu huyo wawa wilaya hiyo akisema,

"Tunamshukuru mkuu wa wilaya na timu yake kwa kuja kutukimbilia, wametusaidia na Mungu awabariki maana tulikuwa hatuna chochote tulikuwa tumebaki watupu lakini mmetusaidia."

Halifa Amiri, mmoja wa waathirika amesema, "Angalau Sasa hivi tumepata nguvu kwasababu tulikwama kwa hiyo sasa hivi  tuna unafuu kidogo, tunamshukuru mkuu wa wilaya yetu kwa kutukimbilia."