DC Siha atoa agizo kwa watendaji kata, vijiji

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro (DC), Thomas Aposn, (katikati) akiwa kwenye kikao maalumu cha kamati ya ushauri wa maendeleo ya Wilaya (DCC).

Muktasari:

Watendaji wa kata na vijiji katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusimamia maazimio ya Baraza Madiwani wa Halmashauri hiyo ya kudhibiti mifugo inayopitishwa na kuharibu barabara zinazojengwa na kuweka njia zatakazotumika kwa ajili ya mifugo hiyo.

By Bahati Chume, Mwananchi [email protected]

Siha. Watendaji wa kata na vijiji katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusimamia maazimio ya Baraza Madiwani wa Halmashauri hiyo ya kudhibiti mifugo inayopitishwa na kuharibu barabara zinazojengwa na kuweka njia zatakazotumika kwa ajili ya mifugo hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Siha (DC), Thomas Apsoni wakati akizungumza katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) kilichokuwa kikijadili bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo viongozi hao walitakiwa kusimamia maazimio hayo ili kulinda miundombinu hiyo.

Apson anasema Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo hivyo ni muhimu kutunza miundombi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu

"Hapa Meneja wa Tarura Wilaya anasema alishatoa muongozo kwa kuwaandikia barua wetendaji wa kata na vijiji kupitia Baraza la Madiwani kuhusu usimamizi wa barabara katika maeneo yao hili mnatakiwa kulisimamia kulinda barabara hizo" ameagiza Apson

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) Wilaya ya Siha, Mhandisi Protasi Kawishe amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la uharibifu wa miundombinu ya barabara linalochangiwa na wananchi kupitisha mifugo huku akitaka wafugaji watumie njia mbadala kupitisha mifugo.

"Sheria ya barabara mifugo ikikamatwa faini ni Sh5, 000 hii sheria inafanyiwa marekebisho mwaka huu inaweza kufikia faini Sh50, 000 kwa sababu inaendana kwenye uhujumi uchumi, kuharibu barabara ni uhujumu uchumi" amesema meneja huyo wa Tarura Kaweshe

Amesema barabara hizo ambazo zipo kwenye kiwango cha changarawe zisipoitishia mifugo zinauwezo wa kudumu hadi miaka mitatu ndipo irudiwe kufanyiwa marekebisho lakini ikipitisha mifugo haiwezi kumaliza hata mwaka mmoja.

“Tunajua mifugo ni muhimu, lakini miundombinu ya barabara nayo tunaihitaji katika matumizi ya kila siku hivyo nawaomba watendaji wote panoja na wafugaji tushikiriane ili tufikie lengo moja la maendeleo ya Wilaya” amesema Kaweshe