Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango ataja siri kuwapo imani potofu katika dini

Dar es Salaam. Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema kuna wimbi kubwa la mafundisho potofu ya kidini yanayochochewa na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Dk Mpango amebainisha hayo leo Septemba 10, 2023  mkoani Iringa katika adhimisho la ibada ya misa takatifu ya Jubilei ya miaka 50 ya Upadre wa Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.

Amesema kuenea kwa misimamo mikali ya kidini inayosababisha baadhi ya watu kujitoa muhanga na kupoteza maisha yao huku akieleza hata nchini wapo wahubiri wa miujiza na wamekuwa wakijilimbikizia mali binafsi kutokana na sadaka za waumini na wananchi wanyonge wenye shida.

“Wananchi wenye shida kama magonjwa, migogoro katika ndoa, kukosa watoto, ajira, umaskini na mambo mengine na bahati mbaya wahanga wengi wa mafundisho hayo potofu ni akina mama,”amesema

Ameongeza kuwa kuna wahubiri ambao kwa uwazi na bila kificho wamekuwa vinara katika kushabikia matendo maovu kama mapenzi ya jinsia moja.

“Sababu ya kuenea kwa kasi mafundisho potofu ni kukua kwa kwa matumizi ya teknolojia, naomba viongozi wangu wa dini zote kutumia teknolojia hiyo kukemea imani potofu na kutangaza neno la mungu na kuwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidi,”amesema.

Changamoto ya pili ametaja kasi ya mmomonyoko wa maadili katika jamii unaoshuhudiwa miongoni mwa wazazi, walezi na hata vijana na watoto.

“Tunashuhudia kuongezeka kwa mauaji ya kikatili, kuzuka kwa vikundi vya vijana vya kihalifu, biashara ya madawa ya kulevya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na ongezeko la familia ya mzazi mmoja na waliozaliwa nje ya ndoa,” amesema.