Dk Mpango azungumzia ushirikiano utunzaji Ziwa Tanganyika

Muktasari:

  • Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kushirikiana na nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kuhakikisha rasilimali zinadumu na kunufaisha wananchi wa nchi husika.

Kigoma. Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kushirikiana na nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kuhakikisha rasilimali zinadumu na kunufaisha wananchi wa nchi husika.

 Akizungumza leo Alhamisi Desemba 16,2021 mjini Kigoma wakati akifungua mkutano wa tisa wa tathmini ya mkataba wa usimamizi endelevu wa rasilimali za ziwa hilo uliowkautanisha mawaziri wa mazingira kutoka nchi nne zinazozunguka  Ziwa Tanganyika, amesema uharibifu wa mazingira unachangiwa na shughuli za binadamu.

Amesema nchi hizo nne ambazo ni Tanzania, Zambia, Burundi na Congo DRC zitaweza kushirikiana kwa pamoja kusimamia uvuvi uliopitiliza, uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira katika Ziwa Tanganyika.

"Kuna haja ya nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika kuwa na kanuni za pamoja ya utunzaji wa mazingira hatua itakayosaidia kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira,"amesema Mpango.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Chande amesema tangu kupitishwa kwa mkataba huo wa usimamizi endelevu wa Ziwa Tanganyika, wameweza kuwa na mafanikio ikiwemo kuanzishwa kwa sekretalieti  ya mamlaka ya ziwa hilo iliyopo Bunjumbura nchini Burundi.

Mkurugenzi wa uvuvi na ufugaji wa samaki wa mamlaka wa Ziwa Tanganyika, Beatrice Marwa amesema kumekuwa na athari mbalimbali zinazojitokeza katika zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kibinadamu na ongezeko la watu wanaotumia rasilimali za ziwa.
[5:27 PM, 12/16/2021] +255 763 349 737: CUF hali si shwari
Tuzo Mapunda, Mwananchi
[email protected]
Dar es Salaam.  Wajumbe wa kamati tendaji ya CUF Wilaya ya Kinondoni na ile iliyovunjwa kwa tamko la mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba wamegombania kutumia ofisi ya wilaya huku kila upande ukidai una haki ya kuitumia.
Katika Mvutano huo uliotokea leo Alhamisi Desemba 16,2021, kundi la wajumbe wa kamati iliyovunjwa na Lipumba Desemba Mosi, 2021 kwa madai ya makosa mbalimbali ikiwemo kushabikia viongozi ngazi ya Taifa kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii,  limesema  bado ni viongozi halali kwa sababu hawajapewa barua rasmi inayoonyesha nafasi walizoshika zimekoma.
Kundi la pili la wajumbe walioteuliwa juzi na Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Kinondoni wanasema wao wana uhalali wa kutumia ofisi hiyo kwa kuwa wanatambulika na mwenyekiti wa chama hicho.
Hata hivyo, mkurugenzi wa habari, uenezi na mahusiano ya umma wa chama hicho, Mohamed Ngulangwa amesema wanaitambua kamati mpya iliyoteuliwa akibainisha kuwa madai ya kamati iliyovunjwa hayana mashiko.
“Katiba yetu ipo wazi mamlaka ambazo zilikuteua kwa kutambua sababu basi inawajibika kuvunja na hupewi barua kwa sababu ni nafasi za kisiasa. Na kama wanaleta vurugu tunajua ni kundi la wahuni tunasubiria taarifa rasmi kwa viongozi tuwachukulie hatua,"amesema Ngulangwa.
Akizungumza na Mwananchi Digital baada ya vurugu hiyo katibu wa kamati iliyovunjwa, Suleiman Masahuni amesema wao bado ni viongozi halali,”tuna uhuru wa kuendelea kutumia ofisi hii na kueendelea kukijenga chama na tangu mwenyekiti kutoa tamko lake la kuvunja kamati Bbado hatujapewa barua rasmi ya kusitisha utendaji kazi wetu."
Masahuni amesema migogoro mingi inayoendelea ndani ya chama hicho inasababisha na viongozi wa kitaifa kwa kukumbatia makundi ya wachache badala ya kuangalia imani ya wananchama na uhai wa chama.