Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Tax amwomboleza Balozi Mushy

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax akitoa salamu za rambirambi kwenye mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy.

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy akisema nchi imepoteza kiongozi mnyenyekevu, mwenye upendo kwa watu.


S:

Janeth Joseph na Omben Mjema, Mwananchi


Moshi. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amesema nchi imepoteza kiongozi mnyenyekevu, mwenye upendo kwa watu, mchapakazi na aliyejitoa kwa yeyote aliyehitaji msaada wake.

Waziri Tax ameyasema hayo leo Desemba 20, 2022 nyumbani Kibosho Road, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy wakati akitoa salamu za Serikali katika mazishi ya balozi Mushy.

"Balozi Mushy alikuwa na mchango mkubwa kwa Wizara na Taifa kwa ujumla, maisha yake yalikuwa mfano wa kuigwa kwetu, ameacha alama katika utendaji kazi wake na mioyo ya watumishi wa Wizara, marafiki, ndugu jamaa na marafiki wa ndani na nje ya nchi.

"Nchi imepoteza kiongozi mnyenyekevu, mwenye upendo kwa watu, mchapakazi aliyejitoa kwa yeyote anayehitaji msaada wake hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika nchi yetu,"amesema Dk. Tax

Balozi Mushy alifariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.