Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Tax kuongoza waombolezaji kumuaga Balozi Mushy

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy. Picha na Rajabu Athumani

Muktasari:

  • Balozi Celestine Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari 2022 na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax anatarajiwa kuongoza mazishi ya Balozi Celestine Mushy ambaye atazikwa kesho Desemba 20, 2022 huko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Balozi Mushy alifariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.

Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 19, 2022 kuhusu maandalizi ya maziko ya Balozi Mushy, msemaji wa familia, Dk Kenneth Lema amesema viongozi wengine watakaoshiriki shughuli hiyo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mbarouk Nassor Mbarouk na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Joseph Sokoine.

“Hadi sasa tumepata taarifa rasmi kwamba viongozi wa wizara wakiongozwa na Waziri watahudhuria shughuli ya mazishi. Atakuwepo pia Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu,” amesema Dk Lema.

Kuhusu ratiba ya mazishi, Dk Lema amesema mwili wa marehemu utatoka mochwari katika hospitali ya KCMC kuelekea nyumbani kwake saa 3:00 asubuhi.

Amesema saa 5 asubuhi, ratiba rasmi ya ibada ya mwisho ya marehemu itaanza na kuendelea hadi saa 7 mchana.

Dk Lema amesema kuanzia saa 7 mchana, taratibu nyingine za kiitifaki pamoja na shughuli ya kuaga zitafanyika na baada ya hapo mwili utakwenda kuzikwa.

“Tunatarajia kuzika saa 9 alasiri, maandalizi yanaendelea vizuri, kila kitu kitakwenda sawa,” amesema msemaji huyo wa familia ambaye pia ni shemeji wa marehemu.