Dk Tulia aanza kazi Mbeya, ‘aikwepa’ ofisi ya Sugu

Monday November 23 2020
dk tulia pic

Naibu Spika na Mbunge Wa Jimbo la Mbeya Mjini (CCM), Dk Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kata ya Uzunguni, Mbeya.

Mbeya. Naibu Spika na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini (CCM) Dk, Tulia Ackson ameeleza sababu za kuanza kutumia moja ya ofisi katika jengo la Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kuwa ni kukwepa mlolongo mrefu wa makabidhiano na Mbunge aliyemaliza muda wake, Joseph Mbilinyi (Sugu) kupitia tiketi ya Chadema.

Dk, Tulia amesema leo Novemba 23, 2020 Nyumbani kwake muda mfupi baada ya kuelekea kuanza majukumu yake ya ubunge kwa kusikiliza kero za wananchi.

"Nimelazimika kuanza kazi leo Novemba 23,2020 ili nitekeleze matakwa yangu ya kikatiba ya kusikiliza kero za wakazi wa Mbeya, nikisema nisubiri makabidhiano nitavuta muda mwingi kama mnavyojua, "amesema.

Amesema kuwa amesukumwa kutekeleza majukumu yake katika jengo la ofisi za wilaya huku akisubiri ufike muda wa kukabidhiwa  ofisi na mbunge aliyemaliza muda wake.

Aidha Dk, Tulia ametumia fursa hiyo kueleza vipaumbele atakavyoanza navyo kuwa ni kuboresha miundombinu ya elimu hususan kujenga kiwanda cha taulo za kike ili kuwezesha watoto wa kike kusoma kwa bidii na kuwa na uelewa wa masomo.

Vipaumbele vingine ni kuboresha soko la wafanyabishara wadogo  katika eneo la Uwanja wa ndege wa zamani ambapo tayari jiji limepata hati miliki ikiwa ni pamoja na kuzikatia bima ya afya kaya 1,000.

Advertisement

Amesema amelazimika kuisaidia jamii katika suala la afya kutokana na changamoto mbalimbali za upatikanaji wa huduma  katika hosptali, vituo vya afya na zahanati.

Advertisement