Dogo Janja ahojiwa polisi, adaiwa kushawishi abiria wasipime Covid-19

Dogo Janja ahojiwa polisi, adaiwa kushawishi abiria wasipime Covid-19

Muktasari:

  • Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19.

Dar es Salaam. Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali, wenyeji wanaorejea na wageni kutoka nje wanatakiwa kuwasilisha kipimo kinachothibitisha hawana maambukizi ya Covid-19, huku wanaotoka nchi zenye maambukizi wakitakiwa kupimwa kwa kipimo maalum ambacho kitagharimu Dola 25 za Marekani, sawa na Sh57,500 kwa kila msafiri.

Dogo Janja ahojiwa polisi, adaiwa kushawishi abiria wasipime Covid-19

Inadaiwa kuwa Dongo Janja aliyekuwa akitokea Afrika Kusini alipinga kufanya kipimo hicho ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter msanii huyo wa Bongofleva ameandika, hii nchi Tanzania bado ina uonevu wa kishamba sana, sidhani kama mama yetu Rais Samia Suluhu  anafahamu.. muda huu nafika uwanja wa ndege wa kimataifa nikitokea Afrika Kusini na Afrika Kusini huko  nimepima na nina majibu ya  corona lakini hawayataki wanataka hela kutupima upya.”

“Sasa ndugu zangu wa Tanzania mimi nina hela lakini sitoi hata kumi..., mniletee uji kituo nitakachokuwepo nikikosekana hewani shughulikeni na Polisi wa uwanja wa ndege.”