Dovutwa aibuka, amwagia sifa Rais Samia

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party(UPDP) kwa Fahmi Dovutwa

Muktasari:

  • Dovutwa alivuliwa uenyekiti na uanachama wa UPDP Desemba 2019 akidaiwa kushindwa kujaza nafasi ya Naibu Katibu Mkuu na kutoa msimamo wa kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwaka huo.

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party(UPDP) kwa Fahmi Dovutwa ameibuka na kumpongeza Rais Samia Suluhu kwa utendaji wake huku akisema ameingia katika hisoria ya wanawake watatu duniani waluowahi kushika nyadhifa za juu katika nchi zao.
Dovutwa alivuliwa uenyekiti na uanachama wa chama hicho Desemba 2019 kwa madai ya kushindwa kujaza nafasi ya naibu katibu mkuu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushirikiana na vyama vingine vya siasa  kutoa msimamo wa chama hicho kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa bila idhini ya kamati kuu.
Akizungumza leo Jumatatu, Aprili 12, na waandishi wa habari, Dovutwa ambaye kwa sasa hana chama baada ya kuvuliwa uanachama wake amesema ametoa maoni yake hayo kama mwananchi na mwanasiasa wa siku nyingi.
Dovutwa amesema anaingia kwenye historia ya wanawake waliowahi kuongoza nchi zao na kufanya maajabu akiwemo Waziri Mkuu wa Israel, Hayati Gorda Mayer na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,Hayati Magrete Thatcher.
Wakati Gorder alifanikiwa katika vita ya Magharibi na Mashariki, waziri Magrete amesema alifanikiwa katika vita baridi ya Magharibi wakiwa wanapambana na gaidi Carlos pamoja na  mizozo ya Masharik na kijikuta wanapachikwa majina ya Iron Ladies.
"Sina wasiwasi na Rais Samia kwani ubora wa kiongozi wa ngazi yoyote ni namna anavyopanga au kuteua wasaidizi wake. Ukikosea kupanga wasaidizi au watendaji dhamira yote itaharibika na ukipatia serikali yako au timu yako italeta ushindani katika nyanja za mapambano ya uchumi,siasa,jamii na utamaduni," amesema Dovutwa.
Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo amezungumzia kuhusu mpango wake katika siasa na kueleza kuwa mpaka sasa hana chama isipokuwa milango ipo wazi kwa atakayemuhitaji.