DPP kutoa ushahidi Kisutu leo

DPP kutoa ushahidi Kisutu leo

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Slyvester Mwakitalu anatarajia kutoa ushahidi leo mchana katika Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Slyvester Mwakitalu anatarajia kutoa ushahidi leo mchana katika Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya Jinai namba 99/2021 inayomkabili Joshua  Kamalamo (37) na mwenzake Yahaya Kapalatu(31), wanaokabiliwa na kesi ya kujitambulisha kuwa wao ni maofisa Usalama wa Taifa (TISS) kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Slyvester Mwakitalu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kujitambulisha kwa DPP kuwa wao ni maofisa kutoka Ofisi ya Raisi, Idara ya Usalama wa Taifa, jambo ambalo ni uongo.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa leo Jumanne Agosti 9, 2022 mchana

Endelea kufuatilia Mwananchi