Dubai yaongoza kutembelewa zaidi duniani

Kwa mujibu wa tuzo za mtandao mkubwa zaidi wa masuala ya usafiri duniani Trip Advisor zinazoitwa Travellers’s Choice Awards, Dubai ndio sehemu ya kwanza na maarufu zaidi  inayoshauriwa kutembelewa kwa mwaka 2023.
Washindi wa tuzo hizi waliangaliwa kutokana na ubora na wingi wa maoni kutoka kwa watalii pamoja na ukadiriaji uliofanywa na watalii mbalimbali. Hii pia imehusisha mara ngapi watalii wameulizia hoteli, migahawa n.k katika mtandao huo kwa Dubai.
Sehemu nyingine maarufu zaidi za kutembelewa kwenye top 10 ya chati hizo ni pamoja na Cancun (Mexico), Greek, Mororcco, Dominican Republic na Istanbul (Uturuki).
Kwa mji wa London uliopo Uingereza ambao umeshika namba moja kwa Bara la ulaya umeshika namba tatu katika kiwango cha dunia.
Hata hivyo kwa kwa mujibu wa ripoti ya tuzo hizo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imetajwa katika nafasi ya tatu katika orodha ya vivutio bora vya asili vya utalii duniani jambo ambalo litasaidia kuongezeka kwa utalii Tanzania lakini haya yote yanasababishwa na jitahada za serikali ya Tanzania katika kukuza sekta ya utalii nchini.