Exim Bank inavyosukuma ujumuishaji kifedha kwa kutumia ubunifu wa kipekee

Exim Bank inavyosukuma ujumuishaji kifedha kwa kutumia ubunifu wa kipekee

Muktasari:

  • Mafanikio ya Tanzania kuwa kinara wa huduma jumuishi za kifedha duniani, leo kuwa mfano mzuri wa mageuzi ya kidigitali barani Afrika, hayatokani na jitihada za mtu mmoja bali za pamoja, zikihusisha taasisi kama Benki ya Exim nchini Tanzania

Mafanikio ya Tanzania kuwa kinara wa huduma jumuishi za kifedha duniani, leo kuwa mfano mzuri wa mageuzi ya kidigitali barani Afrika, hayatokani na jitihada za mtu mmoja bali za pamoja, zikihusisha taasisi kama Benki ya Exim nchini Tanzania.


Benki hiyo si taasisi pekee kati ya zinazotoa huduma za kifedha nchini, lakini ni kinara wa huduma za kidigitali za fedha ambazo jitihada zake za ubunifu zimekuwsa na mchango mkubwa katika kushughulikia changamoto za huduma jumuishi za kifedha nchini.
Katika miaka yake 24 ya kushiriki katika uchumi wa taifa na kusaidia kusukumu dira ya maendeleo, Exim Bank imeongoza katika bidhaa za kidigitali na utoaji wa suluhisho la matatizo katika mageuzi ambalo limekuwa na nafasi kubwa katika kuanzisha ikolojia inayostawi ya teknolojia pana ya fedha (fintech).

Jamii isiyotumia fedha taslimu
Zaidi, kwa kutumia uwezo wa kipekee wa kidigitali, Exim inaendelea kuchangia kwa kiwango kizuri kusukuma ajenda ya ujumuishaji makundi mbalimbali katika huduma za fedha, lengo lake kuu likiwa ni kujenga uchumi jumuishi wa kidigitali na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa jamii isiyotumia fedha taslimu katika shughuli za malipo.


Maofisa waandamizi wa benki wanasema hakuna shaka kuwa uwekezaji wa kidigitali na katika teknolojia ya fedha uliofanywa na Exim Bank ni sehemu ya kuwezedsha kila mtu kufikia huduma za fedha ambazo ni nafuu na nzuri nchini kwa kadri iwezekanavyo.
“Upatikanaji na matumizi mapana ya huduma za fedha zenye gharama nafuu unawezekana na unaendelea nchini Tanzania. Sisi hapa Exim Bank tumepewa heshima kuwa sehemu ya ndoto hiyo ya kuwezesha na dira ya maendeleo ya taifa,” anasema Jaffari Matundu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank.
“Exim Bank inatoa bidhaa na huduma kamili zilizobuniwa kukidhi mahitaji ya wateja wa biashara za rejareja, za kampuni kubwa na taasisi. Mteja kuwa katikati ya huduma zetu ndio imekuwa moyo wa kila kitu ambacho Exim Bank inafanya,” alisema Matundu hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Jitihada zetu za ubunifu katika eneo la huduma za kidigitali za kibenki ni sehemu ya juhudi nzima za kushughulikia matarajio ya wateja,” aliongeza ofisa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa taasisi za kifedha kumfanya mteja kuwa sehemu muhimu katika ubunifu, ambao unajumuisha huduma za fedha na benki kidigitali.

Kuongoza kutoa suluhisho


Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Exim Bank imekuwa ikiongoza katika maeneo kadhaa ambayo yamewezesha suala la huduma jumuishi za kifedha nchini. Jitihada hizo, alisema, zinaendelea kubadili jinsi ya kufanya malipo, uwekaji akiba na hata huduma za uwekezaji zinavyotolewa.
Benki hiyo imefanikiwa katika ubunifu kwa kutumia teknolojia ya kiwango cha juu duniani na kutoa bidhaa kwa kumlenga mteja. Iikuwa ni benki ya kwanza kuanzidha kadi za malipo (Credit Cards) wakati zilipoanzishwa huduma za International Debit MasterCard, Visa Platinum, TANAPA na Visa nchini Comoro.
Exim Bank pia ilikuwa ya kwanza Tanzania kuzindua matumizi ya simu za mkononi katika huduma za kibenki kwa kutumia simujanja (smartphones), ilipoanzisha kiotela (Automated Teller Machine au ATM) na kuanzisha mpango jumuishi wa kutoa fedha kwa wanawake.

Baraza la Taifa Ujumuishaji Kifedha
Akizungumzia nafasi ya Exim Bank katika maendeleo ya nyanja ya teknolojia ya fedha, ofisa mwandamizi wa Baraza la Taifa la Ujumuishaji Kifedha (NCFI) alisema habari ya mafanikio ya mageuzi ya kidigitali na ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania haiwezi kukamilika bila ya kutaja msaada na mchango usio shaka wa Exim Bank.


“Tunatambua na kukubali kile walichokifanya na wanaendelea kufanya katika kuendeleza na kusaidia juhudi za taifa kujumuisha waliotengwa katika mfumo rasmi wa kifedha wenye usimamizi,” ofisa huyo wa NCFI aliliambia gazeti la The Citizen katika mahojiano maalum wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, safari ya Tanzania kuelekea huduma jumuishi za kifedha si juhudi za mtu mmoja bali ni mkakati mpana wa kisekta, ambao unategemea ushiriki na mchango wa wadau kadhaa kuufanikisha, ikiwa ni pamoja na sekta binafsi na ya umma.
Mbali na mchango katika kupanua fursa kwa Watanzania kupata na kutumia huduma bora za kifedha, Exim Bank pia inasifika kwa kuwa ya kwanza nchini kutoa huduma za kifedha nje ya nchi na kuweka alama ya huduma za kibenki nje.
Licha ya kuwepo katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara pamoja na Zanzibar, shughuli za Exim Bank nje ya nchi zinapatikana visiwa vya Anjouan, Moheli na Moroni, Uganda, Jamhuri ya Djibout na Ethiopia kupitia ofisi yao iliyopo Djibout.
Hakuna benki nyingine ya Tanzania iliyofikia mafanikio haya kimataifa.

‘Maliza Kirahisi Kidijitali’
Wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka jana, benki ya Exim ilisisitiza matumizi fanisi ya huduma za kidigitali na kuahidi wateja wake suluhisho bora zaidi la matatizo ya teknolojia ya kifedha huko mbele.


Maofisa wake walisema hakuna kitu kitakachoachwa wakati nchi ikijitahidi kuongeza kasi ya kiwango cha ujumuishaji kifedha kupita asilimia 85 ya sasa kwa kuangalia ufikiwaji wa huduma na asilimia 65 kwa kuangalia matumizi yake.
Kama sehemu ya jitihada hizo, katikati ya mwaka jana Exim Bank ilianzisha kampeni nzuri iliyopewa jina la “Maliza Kirahisi Kidigitali” kwa ajili ya kuendeleza ujumuishaji kifedha wa makundi tofauti na kusaidia katika ujenzi wa uchumi usiotumia fedha taslimu nchini.
Akizungumza katika hafla ya kuanzisha kampeni ya masoko, kiongozi wa idara ya rejareja ya Exim, Andrew Lyimo alisema jitihada za kimkakati zinalenga kuhamasisha wateja wao kuingia uchumi usiotumia fedha ambao unawawezesha kufikia huduma na kufanya miamala kidigitali.
“Kampeni inalenga katika kubadilisha tabia ya watumiaji na kusukuma hali inayoendelea ya kuhama kutoka matumizi ya fedha taslimu kwenda katika malipo ya kidigitali, hasa katika kipindi cha sasa cha janga la Covid-19,” alisema Lyimo Juni 22 mwaka jana.
“Kampeni pia inaendana na kusaidia dira ya serikali ya kukuza uchumi usiotumia fedha taslimu mbali na kuhakikisha kuwa wateja wetu wanahudumiwa bila ya kwenda katika matawi yetu,” aliongeza.

Silaha katika ushindani
Ili kufanya miamala kuwa fanisi zaidi na isiyo na matatizo, Exim Bank inawapa wateja wigo mpana kufanya maamuzi kwa kurahisisha miamala kidigitali kwa njia ambazo zinaifanya benki hiyo kuwa juu katika ushindani.


Hizo ni pamoja na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi kwa kutumia USSD (Unstructured Supplementary Service Data) au njia inayotumiwa na simu za mkononi kuwasiliana na kompyuta ya mtoaji huduma au programu yake, au kwa njia ya simujanja, kadi, mtandao wa sehemu za malipo (POS), hali kadhalika huduma za benki kwa njia ya mtandao kwa kutumia tovuti au programu tumishi.
Kwa kutumia mtandao mpana wenye matawi 28 kote nchini, uwezeshaji huo unamfanya mteja wa benki kupata huduma muhimu za fedha kokote alipo na wakati wote. Hilo linamuhakikishia nafasi ya kufanya miamala kwa urahisi saa 24, siku saba kwa wiki.

Kufanya kazi leo ili kuboresha kesho
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Stanley Kafu alisema promosheni ya “Maliza Kirahisi Kidijitali”, kama ya mwaka uliotangulia iliyoitwa Cash Management Solutions au ya kuelimisha kuhusu suluhisho la matatizo katika usimamizi wa fedha, ililenga kusogeza huduma bunifu za kifedha kwa wateja ambao wanaongezeka.


“Kwa kutumia huduma za kidigitali, wateja wanaweza kufikia akaunti zao, kufanya miamala ya kibenki wakiwa nyumbani au sehemu nyingine yoyote na hivyo kuwa na muda mwingi zaidi wa kufanya mambo mengine muhimu katika kazi au maisha yao ya kila siku,” alisema.
Kampeni ya Cash Management Solutions ililenga kuwezesha wateja kufikia bidhaa zilizowalenga kama vile Cash-In-Transit (usafirishaji wa fedha taslimu na vitu vya thamani kutoka kwa mteja hadi benki na kinyume chake kwa kutumia magari yenye askari wenye silaha), Host-to-Host (wateja kutumia mtandao mpana wa matawi nchini kupokea malipo ya fedha taslimu, hundi au uhamisho wa fedha kutoka kwa wateja wao na vitu vingine huku upatanisho wa taarifa ukijiendesha), Corporate Cheque Captur na huduma za mashine za kuwekea fedha.
“Kila siku Exim Bank iko kazini leo kwa ajili ya kesho bora zaidi na inafanya hivyo kwa kutoa uhuru zaidi wa huduma za kifedha,” alisema Kafu.