Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye Athanas Mrema azikwa Rombo, mamia wamlilia

Mkaburi ya familia ya Athanas Mrema ambaye amezikwa eneo moja na mwanaye na mjukuu wake. Picha Janeth Joseph

Muktasari:

  • Mamia ya wananchi katika Kitongoji cha Kirungu Mokala, Kata ya Kelamfua Mokala wilayani Rombo wamejitokeza kwenye mazishi ya marehemu Athanas Mrema (59) ambaye amezikwa yeye na mwanaye mmoja na mjukuu wake katika eneo moja, huku wengine wakizikwa katika maeneo tofauti jirani.

Rombo. Mamia ya wananchi katika Kitongoji cha Kirungu Mokala, Kata ya Kelamfua Mokala wilayani Rombo wamejitokeza kwenye mazishi ya marehemu Athanas Mrema (59) ambaye amezikwa yeye na mwanaye mmoja na mjukuu wake katika eneo moja, huku wengine wakizikwa katika maeneo tofauti jirani.

 Mazishi hayo yamefanyika leo Februari 6, katika kitongoji hicho ambapo miili ya ndugu wengine inatarajiwa kuzikwa kesho Jumanne na keshokutwa Jumatano katika maeneo ya Keryo, Shimbi na Keryo wilayani humo.

Ajali hiyo iliyoua watu 14 wa familia moja kati ya 20 ilitokea Februari 4,  katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, wilayani Korogwe, Barabara ya Segera - Buiko mkoani Tanga.

Ndugu hao pamoja na majirani walikuwa  wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema(59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es Salaam kuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ndipo walipokutana na ajali hiyo  mbaya.