India, Sri Lanka wajadiliana masuala mbalimbali

Tuesday February 23 2021
majadiliano pic
By Mwandishi Wetu

Sri Lanka. Naibu Balozi wa India, Vinod Jacob amekutana  na wabunge wa Sri Lanka, Mano Ganesan na Palani Thigambaram kujadili masuala  ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa ubalozi wa India nchini Sri Lanka, walijadili masuala yanayohusu wamiliki wa asili ya India pamoja na ushirikiano wa maendeleo kwa kuzingatia utekelezaji wa haraka wa miradi ya nyumba katika maeneo ya shamba.

"Naibu Balozi, Vinod Jacob alikutana na wabunge Mano Ganesan na Palani Thigambaram. Walijadili masuala yanayohusiana na asili ya India pamoja na ushirikiano wa maendeleo kwa kuzingatia utekelezaji wa haraka wa miradi ya nyumba katika maeneo ya shamba," umesema ubalozi wa India nchini Sri Lanka kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mano Gansesan pia aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema alifanya mazungumzo mazuri kwenye mkutano na chakula cha mchana na mkuu wa DHC wa India, Vinod Jacob juu ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Advertisement