Ishirini kidato cha kwanza wajawazito

Ishirini kidato cha kwanza wajawazito

Muktasari:

Zaidi ya wanafunzi 20 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Serengeti wamebainika kuwa na ujauzito na watuhumiwa wanne wa tatizo hilo wamekamatwa, mmoja wao akifungwa miaka 30 jela.

  

Serengeti. Zaidi ya wanafunzi 20 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Serengeti wamebainika kuwa na ujauzito na watuhumiwa wanne wa tatizo hilo wamekamatwa, mmoja wao akifungwa miaka 30 jela.

Jumla ya wanafunzi 5,706 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kati yao wasichana ni 2,683.

Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya wilaya alisema mimba ni tatizo kubwa linaloathiri masuala ya elimu kwa watoto wa kike lakini baadhi ya viongozi katika maeneo yao hawachukui hatua.

“...Mwaka jana wakati wa likizo ya corona kulitokea watoto zaidi ya 28 wa sekondari na msingi kupata ujauzito sasa hivi hawa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 20 wamebainika kuwa na mimba,” alisema akimtaka mwendesha mashtaka kuharakisha kesi zinazohusiana na suala hilo, wakato mojawapo ya aliyemzuia mwanafunzi kwenda shule ili amuoe, akiwa amefungwa miaka 30 jela.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Ayubu Makuruma alisema hawatakubaliana na wanaokatisha masomo hivyo akaomba hatua kali zichukuliwe.