Jela miaka 30 kwa kumbaka binti wa miaka 14

Thursday March 04 2021
MAHAKAMA PIC
By Suzy Butondo

Shinyanga. Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga imemhukumu Zacharia Samweli (59) maarufu Balozi  kifungo cha miaka 30 jela  kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 14.

Hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, Ushindi Swalo akisoma hukumu hiyo amesema amejiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo shaka na kumtia hatiani mtuhumiwa.

“Kitendo cha ubakaji kimekuwa kikifanywa na baadhi ya wanaume wengi wengine hubaka watoto wadogo hili litakuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo,” amesema Swalo.

Mwendesha mashtaka wa Serikali,  Venance Mkonongo akisaidiwa na Wampumbulya Shani amesema binti huyo alianza kubakwa tangu Januari2016 katika mtaa wa Mshikamano ambako wazazi wake wamepanga.        

Inadaiwa wazazi wa binti huyo walikuwa wamepanga katika nyumba ya Samweli na alianza kumrubuni binti huyo na kuanza kumbaka kwa nyakati tofauti kwa kipindi kirefu.

Kesi  ya ubakaji ilifunguliwa Machi 5, 2020 na kutolewa hukumu jana Jumatano Machi 3, 2021.

Advertisement
Advertisement