Jela miaka 30 kwa kumbaka, kumpa ujauzito mwanafunzi

Muktasari:

  • Mkazi wa Veta Mkoa wa Mbeya, Deus Peter (25) amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne.

  





Mbeya. Mkazi wa Veta Mkoa wa Mbeya, Deus Peter (25) amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne Oktoba 13, 2021 na Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Andrew Peter baada ya upande wa mashtaka kujiridhisha na ushahidi wa pande zote mbili.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, wakili Hebel Kihaka akisaidiana na wakili Zena James amesema mtuhumiwa alitenda makosa mawili la ubakaji na kumsababishia ujauzito mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa).

Tukio hilo limetokea kati ya Septemba 2020 na Aprili 2021 huku mtuhumiwa akijua ni kinyume cha sheria.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa amekuwa akitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kinyume na kifungu cha sheria namba 130(1) (2)(e) na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.