JICA imeanzisha mafunzo ya KAIZEN kwa lugha ya Kiswahili mtandaoni

Monday April 25 2022
mafunzoopic
By Mwandishi Wetu

Je umewahi kusikia kuhusu KAIZEN?

KAIZEN ni neno la Kijapani lenye  falsafa ya usimamizi ambalo maana yake ni; “Uboreshaji Endelevu.”Limekuwa likitumika nchini kwa ajili ya kuongeza ubora na tija kwa viwanda vya ndani na huduma, ikiwa ni mradi wa pamoja kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) tangu 2013.

Makao Makuu ya JICA yalizindua  Mafunzo ya Mtandaoni ya KAIZEN mwaka 2021. Ofisi ya JICA Tanzania ilizizindua mafunzo hayo kwa lugha ya Kiswahili kupitia mtandao rasmi wa YouTube ya JICA. Wataalamu wa Kijapani wa KAIZEN wanaeleza na kutambulisha mbinu na kutoa mifano ya kampuni za Kijapani zinazotekeleza mbinu za KAIZEN kwa ukamilifu kupitia  mafunzo hayo.

1. Mkakati wa Usimamizi

2. Uhasibu

Advertisement

3. Usimamizi wa Ubora

4. Trela

JICA inaamini kuwa nyenzo hii inaweza kusaidia mtu yeyote anayetaka kuboresha tija, ubora na faida.

Marejeleo:

Tuzo za KAIZEN mwaka 2021

<https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/supplement/congratulations-outstanding-tanzanian-companies-awarded-the-5th-kaizen-award-competition-3316620>

Mkutano wa Mwaka wa KAIZEN 2021 jijini Dar es Salaam

<https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/supplement/the-largest-international-event-for-kaizen-in-africa-was-held-in-dar-es-salaam-3581090>

Tuzo za KAIZEN mwaka 2022

<https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/supplement/outstanding-tanzanian-companies-awarded-in-the-6th-tanzania-kaizen-award-competition-3752952>

Mradi wa NINJA- Kwa ajili ya kuhamasisha kampuni za Kitanzania kukuza biashara zao

<https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/supplement/three-tanzanian-innovative-startups-with-documentary-videos-3743402>

Kuhus JICA

Shirika lililokasimiwa jukumu la kusimamia ODA (Msaada Rasmi wa Maendeleo). Ni mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya misaada duniani yanayosaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi zinazoendelea duniani. Nchini Tanzania, JICA imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Tanzania kwa takriban miaka 60 katika sekta nyingi kama vile Kilimo, Viwanda, Miundombinu n.k tangu 1962.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Ofisi ya Tanzania

SLP 9450, Dar es Salaam, Simu: 022-211327/30

<https://www.jica.go.jp/tanzania/english/index.html>Advertisement