Jifunze lugha ya Kifaransa na utamaduni wake kupitia taasisi za Alliances Françaises nchini

Onyesho la burudani la Tarajazz maalumu kwa ajili ya Tamasha la Vitabu na Uandishi la Taasisi ya Alliance ya Arusha, lililofanyika Novemba 2020.

Muktasari:

  • Mtandao wa Alliance Françaises umeanzishwa mwaka 1883, ni mdau mkubwa wa diplomasia ya utamaduni wa Ufaransa huku lengo la kuanzishwa kwake likiwa ni kukuza lugha ya Kifaransa na utamaduni wa Kifaransa kwa nchi zingine.

Mtandao wa Alliance Françaises umeanzishwa mwaka 1883, ni mdau mkubwa wa diplomasia ya utamaduni wa Ufaransa huku lengo la kuanzishwa kwake likiwa ni kukuza lugha ya Kifaransa na utamaduni wa Kifaransa kwa nchi zingine.

Mtandao huo umekuwa kwa kiasi kikubwa katika miaka kadhaa iliyopita na sasa ndiyo mtandao wa utamaduni unaoongoza duniani, ukiwa na matawi katika zaidi ya nchi 135. Nchini Tanzania, taasisi ya kwanza ya Alliance Françaises ilianzishwa mwaka 1961 jijini Dar es Salaam, baadae ikafuatiwa na ile ya Arusha na kisha Association Franco- Zanzibarite (AFZ), huko Stone Town.

Taasisi hizi zisizojiende-sha kwa faida zina dhamira kuu mbili. Kwanza, kukuza na kufundisha lugha ya Kifaransa hapa nchini. Zikiwa ni taasisi za mafun-zo, Alliance Françaises zina timu ya walimu waliobo-bea, wenye hamasa na walio tayari kusambaza mapenzi na maarifa yao ya lugha hiyo kwa wengine.

Kila mwaka, zaidi ya wanafunzi 1,000 wanajiandikisha kuhudhuria masomo ya lugha ya Kifaransa katika taasisi zake zote tatu za Alliance mwaka mzima. Kila mwa-nafunzi anaweza kujisajili kwa kuwa vipindi hupangwa kulingana na ngazi ya elimu ya mwanafunzi husika.

Watoto, vijana na watu wazima wanaweza kuchagua kusoma kozi za miezi mitatu. Pia, wanafunzi wanaweza kutumia maktaba ya utamaduni wa Ufaransa, ikiwamo jukwaa la kimtandao ambalo limejaa filamu na riwaya zilizo katika lugha ya Ufaransa.

Maktaba hii inawasaidia wanafun-zi kuimarisha ujuzi wao wa lugha na kukuza maarifa yao ya utamaduni wa Ufaransa. Kwa kuongezea, Alliance ni vituo vya mitihani kwa ajili ya kutoa vyeti vya lugha ya Kifaransa kama vile DELF au TEF. Vyeti hivi mara nyingi huwa ni muhimu na lazima hasa unapokwenda kusoma au kufanya kazi nje ya nchi katika nchi ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa kama vile Ufaransa au Canada.

Pia, Alliance Françaises ni vituo ya utamaduni, ambavyo vimekuwa vikiandaa matukio mbalimbali ya kiutamaduni kwa mwaka mzima. Jiji la Arusha hivi karibuni liliandaa Tamasha la Vitabu na Uandishi wakati jiji la Dar es Salaam likiandaa tukio la Usiku wa Sanaa, sambamba na matama-sha kadhaa ya muziki, utumbuizaji na semina zikiandaliwa mara kwa mara.

Zikitengeneza muungano baina ya tamaduni na wasanii wa Ufaransa na Tanzania, taasisi hizi zinajihusisha zaidi na asasi za kiraia. Zinachochea mwingiliano wa tamaduni tofauti kwa kuwatangaza wasanii wazawa, wakiwapa fursa na jukwaa la kuonyesha ubunifu wao.

Mbali na uwepo wa matukio haya makubwa, semina, michezo kwa ajili ya watoto au maonyesho ya filamu za Kifaransa, hupangwa kwa kila wiki, ili kila mmoja aweze kutambua utamaduni wa Kifaransa. Taasisi hizi ni sehemu za kuishi na kukutana, na hata kumbi zake zimebuniwa ili kuruhusu watu kubadilishana tamaduni zao.

Taasisi ya AFZ imehamishiwa katika Zahanati ya zamani ya mji wa Stone Town, katikati ya mji, huku ile ya Arusha ikiboresha kumbi zake. Taasisi iliyopo Dar es Salaam, ambayo itasheherekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, hivi kari-buni ilizindua maktaba yake mbele ya Balozi wa Ufaransa nchini, Frédéric Clavier.

Maktaba hii imetengenezwa mahsusi kuwapa watu mazingira mazuri na tulivu kwa wale walio tayari kudadisi na kujifunza utamaduni wa Ufaransa. Bila ya kujali kama unataka kujifunza lugha ya Kifaransa au kukutana na marafiki au familia, unakaribishwa katika taasisi za Alliances Françaises nchini Tanzania,

Bienvenue à tous.