Joe Biden kwa Lady Gaga humuelezi kitu

Joe Biden kwa Lady Gaga humuelezi kitu

Muktasari:

Rais wa Marekani, Joe Biden jana alikula kiapo cha kuwa kiongozi mkuu w nchi hiyo katika tukio ambalo wasanii Jennifer Lopez, Lady Gaga na Garth Brooks walitumbuiza.

Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Joe Biden jana alikula kiapo cha kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo katika tukio ambalo wasanii Jennifer Lopez, Lady Gaga na Garth Brooks walitumbuiza.

Hadi jana Jumatano Januari 21, 2021 wakati Biden, kada wa chama cha Democratic akila kiapo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Twitter alikuwa akiwa follow watu wengine 46 akiwemo Lady Gaga.

Biden alianza kum follow Lady Gaga tangu mwaka 2015 na mara kadhaa wawili hao wamekuwa wakitajana kwenye mitandao yao kutokana na kazi nzuri anazofanya kila mmoja.

Joe Biden kwa Lady Gaga humuelezi kitu

Inaelezwa kuwa ukaribu wao ulianza mwaka 2014 baada ya Biden kuanzisha kampeni ya Its On Us kwa ajili ya kupambana na kumaliza ukatili wa kijinsia.

Mwaka huo Lady Gaga alijitangaza kuwa aliwahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia zamani. Na mwaka 2015 alitangaza kuunga mkono kampeni iliyokuwa inaendeshwa na Biden.

Akaunti rasmi ya Twitter ya kiongozi mkuu huyo inafollow watu 12 akiwemo  mwanamitindo Chrissy Teigen.

Akaunti hiyo inayofahamika kwa jina la @potus ambayo ni kifupi cha President Of The United States ilifollow akaunti ya Teigen jana baada ya kuapishwa.

Kwenye mitandao mingine kama vile Instagram na Facebook, Biden amefollow wasanii wengi tu.

Baadhi ni muigizaji Dwayne Johnson ‘The Rock’, mchekeshaji Micheal Keegan na wanamuziki Jennifer Lopes, Luis Fonsi na Bill Elish.