Kampuni za kuzalisha mbegu zatakiwa kuongeza uzalishaji

Kampuni za kuzalisha mbegu zatakiwa kuongeza uzalishaji

Muktasari:

  • Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSC) imebainisha kwamba kuwa zipo kampuni nyingi zikiongeza kasi ya kuzalisha mbegu zitapunguza uingizaji wa mbegu kutoka nje ya nchini.

Mtwara. Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSC) kanda ya kusini, imezitaka kampuni zinazozalisha mbegu kuongeza nguvu katika uzalishaji wa mbegu hizo ili kupunguza uingizaji wa mbegu kutoka nje ya nchi.

Akizungunza wakati wa maonyesho ya nanenane kanda ya kusini, meneja wa Taasisi hiyo, Dickson Rwabulala amesema endapo kampuni zitaongeza nguvu katika uzalishaji na kuwa na uwezo mkubwa, itasaidia wakuwalima nchini kuondokana na matumizi ya mbegu zinazotoka nje ya nchi.

Amesema kuwa zipo kampuni nyingi zikiongeza kasi ya kuzalisha mbegu zitapunguza uingizaji wa mbegu kutoka nje ya nchini.

“Sawa mbegu zingine zinakuja na vibali vyote na zimeshakaguliwa lakini tunao watalaamu hapahapa nchini wanajua mazingira yetu hali yetu ya hewa ni vema uwezo ukaongezeka ili kuweza kudhibiti uignizaji wa mbegu kutoka nje.

“Sisi kazi yetu kubwa ni kukagua na kufundisha na kusimamia biashara ya mbegu Tanzania kwa wanaohifadhi kuuza na kuzalisha mbegu nchini ambapo tunachukua sampuli ili kuangalia uotaji na sampuli ya mbegu hiyo.

“Pia, tunamshauri mkulima anapopata pembe aangalie nembo na kufuata maelekezo ili kujua ni mbegu sahihi zimepitia TOSC ambapo pia hata kwa wazalishaji wa miche pia tunato elimu kwa wzalishaji wa miche ya mikorosho na matunda ili kupata mbegu bora zisizo na magonjwa,” amesema.

Amesema mara nyingi kaguzi zinafanyika lakini sio kwa kutoa taarifa, wanafanya kwa kushtukiza ili kusaidia kubaini mbegu zisizo sahihi katika maduka na kubaini udanganyifu unaoweza kufanywa na waingizaji na wauzaji wa mbegu.

“Ili kuweza kuweza kumuwajibisha mtu lazima afahamu kwanini anawajibishwa kwahiyo tunatoa elimu kwa wafanyabishara kwa kuwapa mafunzo ili kujua sheria, kanuni zitakazo muongoza katika uingizaji na uuzwaji wa mbegu,” amesema Rwabulala.

Kwa upande wake, mkulima kutoka wilaya ya Lindi, Fatuma Hamis alisema kuwa elimu hiyo itaenda kuwasaidia ili waweze kuachana na utunzaji wa mbegu baada ya kuvuna mazao ambazo hazizingatii vigezo wala sheria.

“Unajua wakulima wengi hatuna uelewa wa mbegu tukilima tukivuna tunatunza mbegu hatujua kama kuna sheria na vigezo sisi tunajua tu kuwatunza kuvuna lakini sasa tunaelewa kuwa zipo mbegu ambazo zimedhibitishwa na watalaamu na tunapaswa kuzitumia hizo” alisema