Kashmir wapiga kura muhimu kumaliza mzozo wa muda mrefu

Kashmir wapiga kura muhimu kumaliza mzozo wa muda mrefu

Muktasari:

Kashmir, India. Ushiriki mkubwa wa watu hasa vijana na wanawake katika jimbo la Kashmir katika uchaguzi wa mabaraza ya maendeleo katika majimbo (DDC) katika Muungano wa jimbo la Jammu na Kashmir unaweza kubadilisha maisha ya watu katika jimbo hilo.

Kashmir, India. Ushiriki mkubwa wa watu hasa vijana na wanawake katika jimbo la Kashmir katika uchaguzi wa mabaraza ya maendeleo katika majimbo (DDC) katika Muungano wa jimbo la Jammu na Kashmir unaweza kubadilisha maisha ya watu katika jimbo hilo.

Kitendo cha watu wengi kujitokeza katika uchaguzi huo ni ishara ya kuhusika kwao na kujitoa kutoka kwenye mzunguko wa vifo na uharibifu uliokithiri kwa watu wasio na hatia katika jimbo la Kashmir.

Wananchi wameamua kufuata ajenda ya maendeleo na kuboresha siasa za nchi. Uchaguzi wa DDC ni wa kwanza katika Jammu na Kashmiri baada ya mabadiliko ya ibara ya 370 ya Katiba yaliyofanywa na Serikali kuu Agosti 5, 2019 baada ya kutokea machafuko.

“Watu wana matumaini makubwa kwa wawakilishi waliowachagua ambao watawaletea maendeleo na ndiyo maana uchaguzi huu ni muhimu kama msingi wa chimbuko la ajenda ya baadaye na kutoka kwenye utengano na mapigano ya kijeshi,” walisema wapiga kura walioshiriki uchaguzi huo.

Demokrasia ni mfumo mzuri kama hatua ya kupinga siasa za kujitenga na kuwa na mapigano ya wanamgambo.

Ushiriki huo wa wapigakura unalenga kuimarisha uwakilishi toka ngazi ya chini. Uchaguzi huo ni fursa kwa watu kuueleza ulimwengu kwamba Wakashmir wanataka amani na kujitoa kwenye vifo na uharibifu uliokuwa ukisababishwa na wanamgambo kwa miongo mitatu iliyopita.

Licha ya kwamba wananchi katika jimbo hilo wanatatizwa na kutokutekelezwa kwa ibara ya 370 ya kugawanyika kwa jimbo la Jammu na Kashmir katika muungano wa majimbo ya utawala.

Inachukuliwa kama tusi kubwa kwa historia na hadhi ya Wakashmiri katika muungano wa India waliyopewa na kukubaliwa na Bunge la India. Hata hivyo, watu bado wana imani na demokrasia taasisi za kikatiba katika nchi.

Malengo yaliyotolewa na viongozi wa sasa katika kutekeleza ibara ya 370 yalikuwa kwamba utawala wa kijeshi ungekoma, demokrasia ingeimarishwa, mshikamano wa Kashmiri kufufuliwa, fursa za ajira kuanzishwa kwa vijana.