Kauli ya Master J kuhusu wanaomchukulia poa Diamond Platnumz

Kauli ya Master J kuhusu wanaomchukulia poa Diamond Platnumz

Muktasari:

Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Master J amesema huwa anawashangaa watu wanaomchukulia poa msanii Diamond Platnumz  licha ya kuwa ana mchango mkubwa katika muziki wa Bongofleva.

Dar es Salaam. Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Master J amesema huwa anawashangaa watu wanaomchukulia poa msanii Diamond Platnumz  licha ya kuwa ana mchango mkubwa katika muziki wa Bongofleva.

Ameeleza hayo katika mahojiano na Mwananchi Digital iliyotaka kupata maoni yake kuhusu wasanii wa Bongofleva  walivyowaburuza wasanii wa Afrika Mashariki katika tuzo za Afrimma.

Walioibuka kidedea katika tuzo hizo ni Diamond, Nandy na Zuchu.

Amesema  unapozungumzia muziki wa Tanzania kufanya vizuri na kusikika kimataifa hadi kutwaa tuzo kubwa ikiwemo ya Afrimma huwezi kuacha kumtaja Diamond Platnumz, “ninakerwa namna baadhi ya watu wanavyomchukulia poa msanii Diamond..., kapambana kubadili muziki wa Bongofleva, kwani ni moja ya wasanii aliyejipenyeza kwenye soko la muziki wa Nigeria ambao wenzetu tayari wametangulia kwenye muziki siku nyingi.”

“Mpaka leo tunaona wasanii wa Nigeria wanavyokuja kila siku hapa nchini na pia kuwakimbiza washindani wetu wakiwemo Kenya na Uganda, ambao zamani walikuwa wanatuona hatujui muziki na wa kutwaa tuzo kila uchwao huku sisi tukibaki watazamaji .”

Kauli ya Master J kuhusu wanaomchukulia poa Diamond Platnumz

Master J ambaye amewasaidia wasanii wengi kufanikiwa katika muziki, “lakini sasa heshima hiyo imekuja kwetu mpaka kufikia hatua ya kuona kama tunabebwa, bila kujua kwamba Watanzania tuliangalia wapi tumejikwaa tukakubali kujifunza kupitia wao na nchi nyingine kwa kwenda kuangalia wanafanyaje ikiwemo ubora wa  video za muziki wao na katika hili wasanii kama Diamond huwezi kuacha kutaja mchango wao hivyo asichukuliwe poa kihivyo.”