Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi wanaopinga kutozwa faini Ngorongoro kusikilizwa Mei 10

Muktasari:

  • Wananchi hao wawili wanadai kutozwa faini ya Sh15 milioni na NCAA Januari 25, 2023 baada ya kukutwa wameingiza mifugo katika pori Tengefy la Pololeti, akisema ni kinyume na Sheria ya mamlaka hiyo.

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Mei 10, 2023 kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na wakazi wawili wa wilaya ya Ngorongoro wanaopinga utozaji wa Sh15 Milioni kama faini baada ya kuingiza mifugo katika pori tengefu la Pololeti.

Waomba rufaa katika rufaa hiyo ya jinai namba 9/2023 ni Baraka Kesoi anayedai kutozwa Sh13 milioni na Baraka Oloishiro aliyedai kutozwa Sh2 milioni baada ya kudaiwa kuingiza ng'ombe, mbuzi na kondoo kwenye pori hilo, ambapo wamedai kutozwa faini Sh 100,000 kwa ng'ombe mmoja na Sh25,000 kwa kila mbuzi na kondoo.

Kesoi na Oloishiro wamewakilishwa na mawakili Joseph Ole Shangai na Dennis Mosses huku wajibu rufaa ambao ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Mkurugenzi wa wanyamapori na Jamhuri, wakiwakilishwa na Wakili wa Serikali Tonny Kilomo.

Leo Jumatano Aprili 5, 2023 mbele ya Jaji Mohamed Gwae, shauri hilo lililotajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo lilipangwa kwa ajili ya kutajwa ambapo alisema litasikilizwa Mei 10, 2023.

Wakili Mosses ametaja miongoni mwa hoja za rufaa hiyo ni pamoja na waomba rufaa hao kudai NCAA haina mamlaka kutoza faini kwenye sehemu ambazo ni za nje ya eneo hilo ikiwemo eneo la pori tengefu ambalo limeanzishwa na Sheria ya Wanyamapori na kuwa mwenye mamlaka ni Mkurugenzi wa wanyamapori.

Nyingine ni utozaji wa faini ya Sh 100,000 kwa ng'ombe mmoja ni batili na kinyume na sheria, kutoza faini Sh 25,000 kwa kondoo au mbuzi mmoja ni batili na kinyume cha sheria pamoja na faini ya Sh13,000,000  ni kinyume cha kiwango kilichowekwa kisheria.

Wakili huyo amedai Januari 25 mwaka huu waomba rufaa walikamatwa katika pori hilo wakilisha mifugo yao na kutozwa faini hiyo ambapo alidai wana ushahidi wa namba mahususi ya kuweka malipo ya serikali 'control number' waliyodai kupewa na na NCAA pamoja na risiti ya malipo.

"Wanaomba mahakama iseme uamuzi wa NCAA wa kutoza faini ni kinyume cha sheria na faini hiyo ni kiwango cha juu kabisa ambacho kimezidi kilichowekwa na sheria," amesema.