KESI YA UHAINI 1985: Ofisa usalama abanwa na wakili-15 mahakamani, Jaji aingilia kati

Baada ya shahidi wa sita kumaliza ushahidi wake, Januari 25 kesi iliingia katika siku yake ya tano. Kama tulivyoona katika toleo lililopita, shahidi wa sita kwa upande wa mashtaka alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Mhaville, ambaye wakati uliodaiwa kuwa njama za uhaini zilikuwa zinapangwa, yeye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Katika ushahidi wake, Mhaville alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha alipata habari za mshtakiwa Kapteni Christopher Kadego yuko Arusha akitafuta risasi na bunduki za kumuua Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na kupindua serikali yake.


 Kuendelea kusoma habari hii bonyeza hapa: https://egazeti.co.tz/show_related/8729