Kigogo polisi adaiwa kutorosha walionaswa na mali za Sh2.2 bilioni

Mchimbaji Tanzanite mbaroni tuhuma kumpa mimba mwanafunzi

Muktasari:

Ofisa upelelezi wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi.

Mkinga. Ofisa upelelezi wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kukamatwa na mali za magendo zenye thamani ya zaidi ya Sh1.2 bilioni.

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa Tanga, Omary Mgumba alipokuwa akitoa taarifa ya ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa 24 waliokamatwa na magendo ya vitenge.

Mgumba alisema alishangazwa na hatua hiyo na alipofanya kikao na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, ndipo alibaini aliyewaachia huru watuhumiwa ni ofisa upelelezi wa Wilaya Mkinga aliyedai kupokea maelekezo kutoka kwa ofisa upelelezi wa mkoa (bila kutaja majina).

Alisema tayari ofisa huyo amekamatwa na yuko mahabusu uchunguzi unaendelea na ukikamilika hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Nimshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, baada ya kuona yametokea makosa haraka alichukua hatua ya kumuweka ndani na hatua nyingine zitafuata,” alisema Mgumba.

Akizungumzia hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Sophia Jongo alisema amepokea maagizo kutoka kwa mkuu huyo wa mkoa na anaendelea kuyafanyia kazi.