Kikwete aeleza mikakati ya AGRA

Rais wa awamu ya nne na Mjumbe wa Bodi  ya Shirikisho la Mageuzi ya Kijana Tanzania (Agra), Jakaya Kikwete akiangalia ubora wa Mchele uliokobolewa katika Kampuni ya Raphael Group Limited ya  iliyopo Uyole Jijini Mbeya Februari 15, 2022. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

Rais wa awamu ya Nne na Mjumbe wa Bodi ya Shirikisho la Mageuzi ya Kijana Afrika  (Agra)Dk ,Jakaya Mrisho Kikwete amesema wamedhamilia kuleta Mapinduzi ya kijana kwa  kuwekeza kwa  wakulima wadogo

Mbeya. Rais wa awamu ya Nne na Mjumbe wa Bodi ya Shirikisho la Mageuzi ya Kijana Afrika (Agra),Dk ,Jakaya Mrisho Kikwete amesema wamedhamiria kuleta Mapinduzi ya kijana kwa  kuwekeza kwa  wakulima wadogo nchini kwa  lengo la kuwawezesha  kuzalisha kwa tija  na  kuwepo kwa chakula cha ziada kulingana na mahitaji.

Dk Kikwete amesema Februari 15, 2022 mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kutembelea viwanda vya uchakati wa mazao ,ikiwepo  Kampuni ya Raphael group Limited iliyopo kata ya Uyole Jijini hapa na uwekezaji wa shamba lenye ukubwa wa hekari 4,800 lililopo Wilaya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Amesema kuwa tangu kuanza kwa Shirika hilo wamewekeza zaidi kwa   wakulima wadogo na si wa kati na wakubwa  na misaada ya  inayotolewa ni kuwawezesha kuzalisha mazao   ya chakula na biashara ya kimkakati ili  nchi iwe na chakula cha kujitoshereza na wao kunufaika kiuchumi.

''Katika kuona wakulima kuzalisha  mazao   ya kimkakati wanatoa  mafunzo kwa  wataalamu  kupitia Agra katika shahada ya uzamili na nyinginezo  lengo ni kuona wakulima wadogo na kwa   Tanzania wamezalisha  wataalam 42 wataokaosaidia  katika Sekta ya Kilimo.''amesema.

Kikwete amesema kuwa pia wamewekeza kutoa fedha kwa wazalishaji wa mbegu ambao watakuwa chachu ya kuhamasisha wakulima kuwa na tija ya kuzalishaji mazao kulingana na mahitaji ya Taifa na kuwepo na ziada ya chakula.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Raphael group, Raphael Ndelwa ameiomba Serikali kuendelea kuwekeza kwa wakulima wadogo hususan wa zao la Mpunga ili waongeze tija ya uzalishaji.

''Tunaomba sasa Serikali kupitia Agra kuona namna pekee wa kutuoana wawekezaji wa viwanda vya kuchakata na uhifadhi wa Mazao ya chakula na biashara kwa wakulima wadogo wadogo nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Athony Mavunde amesema kuwa kama Serikali imeweka mikakati kusaidia wakulima ili kufikia malengo iliyojiwekea katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kimkakati.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema kuwa kwa Mkoa wa Songwe kuna hekta 4,800  ambazo zinazalisha masao ya kimkakati  kwa ajili ya ambayo yatakuwa na tija kubwa kwa Taifa.

'' Amesema pia kuna eneo lenye ukubwa wa hekta 600 limeachwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kwamba suala la changamoto za nishati ya umeme katika maeneo ya uwekezaji linashughulikiwa.