Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete ahimiza mapambano dhidi ya Ukimwi

Muktasari:

  • Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ametoa wito huo wakati akiwaaga wapanda mlima 36 na waendesha baiskeli 25 kuzunguka Mlima Kilimanjaro kupitia lango la Machame kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kupitia kampeni  ya GGM “Kili Change 2023.”

Hai. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hapa nchini.

Kikwete ameyasema leo Julai 14, 2023 wakati akiwaaga wapanda mlima 36 na waendesha baiskeli 25 kuzunguka Mlima Kilimanjaro kupitia lango la Machame kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kupitia kampeni  ya GGM “Kili Change 2023.”

“Tunavyoshudia hivi leo Serikali imekuwa mstari wa mbele kuunga juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali, inachangia fedha lakini hazijatosha, tunahitaji na wengine nao wachangie na katika wale wanaochangia Serikali inawaunga mkono kama vile mlivyoshuhudia leo Serikali ikishirikiana na GGML katika kampeni ya kutafuta fedha za kupambana na Ukimwi,” amesema Kikwete.

Ameongeza kuwa ushiriki wa wapanda mlima hao ni dhahiri kuwa dhamira yao ya kupambana na ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya sifuri tatu ifikapo mwaka 2030 kwa maana ya sifuri ya kupunguza mambukizi mapya, sifuri ya kupunguza unyanyapaa na sifuri ya vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Nchini (Tacaids), Jerome Kamwela amesema wataendelea kushirikiana na kampuni ya Geita Gold mine (GGMl) ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, tatizo la Ukimwi linamalizika hapa nchini.

“Tunawashukuru wenzetu wa GGM tumekuwa tukishirikiana nao katika kampeni hii ya mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa muda mrefu lengo ni kufikia mahali pazuri na kuhakikisha gurudumu hili ifikapo mwaka 2030 tumemaliza tatizo la Ukimwi hapa nchini,”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong ameishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono katika kampeni hiyo ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi hapa nchini na kwamba lengo lao ni kuona tatizo linamalizika.