Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete ahudhuria mazishi ya Balozi Mushy

Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini  Austria, Celestine Mushy ambaye anazikwa nyumbani kwake Kibosho road, wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili nyumbani kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy kuhudhuria mazishi ya balozi huyo.

Moshi. Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili nyumbani kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy kuhudhuria mazishi ya balozi huyo.


Balozi Mushy alifariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.


Hata hivyo viongozi mbalimbali wa dini pamoja na ndugu jamaa na mafariki wamefika nyumbani hapo kwa ajili ya kumsindikiza katika nyumba yake ya milele.


Mazishi ya Balozi Mushy yanafanyika leo Jumanne Desemba 20, 2022 nyumbani kwake Kibosho road, wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


Balozi Mushy ambaye ameacha watoto wawili na mke aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari 2022 na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.


CCM watoa salamu


Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mazishi hayo, Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka amesema chama hicho kitamkumbuka Balozi Mushy kama nyenzo kuu ya mchango wa maendeleo katika Taifa.


Shaka amesema "Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa katika mchango mkubwa wa Balozi Mushy katika kuimarisha na kuelimisha ushirikiano wa kimataifa hivyo chama kinathamini mchango wake alioutoa,


"Watumishi wengine waliobakia tumesikia Balozi Mushy akizungumziwa wema na mazuri lakini alama aliyoiacha        Balozi Mushy katika maeneo aliyofanya kazi. Ni matumaini yetu mwenzetu ametangulia lakini funzo kwetu kubwa ambalo tumepata nyuma yake ni kwamba tupande na tuweke alama na mbegu ya wema," amesema Shaka na kuongeza.

"Wema huo ni matumaini yetu kwamba watumishi waliobakia wa serikali lakini wa siasa tutaishi katika nyayo ambazo balozi Mushy alipigania," amesema  Shaka