Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete amwomboleza Balozi Mushy

Raisi wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Balozi wa Austria, Celestine Mushy

Muktasari:

  • Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy alikuwa kijana hodari, mahiri, mzalendo katika nchi yake na mwenye umakini wa kidiplomasia.

Moshi. Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy alikuwa kijana hodari, mahiri, mzalendo katika nchi yake na mwenye umakini wa kidiplomasia.

Kikwete ameyasema hayo leo Desemba 20, 2022 nyumbani kwake Kibosho Road, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za rambirambi.

Balozi huyo aliyefariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga baada ya gari lake kugongana na lori la mizigo na kuungua moto, anatarajiw akuzikwa leo mkoani Kilimanjaro.

"Balozi Mushy alijiunga na Wizara ya mambo ya Nje mwaka 1999 mimi nikiwa waziri kipindi hicho, alikuwa ni mmoja wa vijana hodari na kwenye timu yake ya vijana 17 ambao wengi wao ni mabalozi, ilikuwa imeandaliwa vizuri kutokana na uwezo wao," amesema.


Amesema kutokana na utendaji wake mzuri, "Tulimpeleka ubalozi wa New York baada ya Ofisi ya Waziri mkuu wakati ule (Edward) Lowasa kutaka msaidizi, ndipo tukamchukua Mushy tukampeleka kule na badaye aliendelea na (Waziri Mkuu mstaafu- Mizengo) Pinda.

“Wakati huo nilipokuwa Rais, aliyekuwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa tukamwomba Waziri Mkuu Pinda amruhusu Mushy arudi wizarani awe balozi na kuwa Mkurugenzi wa idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,” amesema.

Kikwete amesema hata Rais Samia alipomteua kuwa balozi wa Austria hakushangaa kutokana na utendaji wake mzuri.

"Nilifurahi kuona Rais amemteua mtu mwenyewe kuwa balozi wa Austria na sikushangaa alipoteuliwa," amesema Kikwete.