Kina Mbowe wakwama tena, mapingamizi yagonga mwamba

Muktasari:

Katika kesi hiyo ndogo mawakili hao wa mshtakiwa huyo walipinga kupokewa maelezo hayo akitoa hoja mbalimbali huku akiungwa mkono na mawakili wengine wa utetezi.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Devisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayohusu maelezo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Mohamed Abdillah Ling’wenya.

Mapingamizi hayo yaliwekwa na mawakili wa mshtakiwa huyo, Fredrick Kihwelo na Dickson Matata.

Katika kesi hiyo ndogo mawakili hao wa mshtakiwa huyo walipinga kupokewa maelezo hayo akitoa hoja mbalimbali huku akiungwa mkono na mawakili wengine wa utetezi.

Pamoja na mambo mengine mawakili wa utetezi walipinga kupokewa maelezo hayo kwa madai kuwa mshtakiwa huyo hakutoa maelezo kituoni hapo, kwa kuwa hajawahi kufikishwa kituoni hapo na kwamba hakuwahi kutoa maelezo yake popote.

Mapingamizi hayo yametupiliwa mbali leo Jumanne Desemba 14, 2021 na Jaji Joachim Tiganga ambaye amesema hoja zote za utetezi zimetupiliwa mbali hivyo maelezo haya yanapokewa.

Hapa ni sehemu ya mwenendo wa Jaji Joachim Tiganga akitoa uamuzi;

Jaji Tiganga tayari ameingia mahakamani kwa ajili ya kuanza kusoma uamuzi na mawakili wa pande zote wanajitambulisha

Wakili wa Serikali Mkuu, Robert Kidando: Shauri hili linakuja kwa ajili ya kutolea uamuzi, tuko tayari.

Wakili Peter Kibatala: Nasi upande wa utetezi tuko tayari

Jajj Tiganda anarekodi mwenendo wa leo, na ukumbi uko kimya ukisubiri kusikia sauti yake.

Jaji Tiganga anaanza kusoma uamuazi kwa kutoa muhtasari.

Jaji Tiganga: Shauri hili ni kweli linakuja kwa ajili ya uamuzi ambao ulikuwa reserved.

Anaanza kutoa historia ya shauri hili dogo ambalo linatolewa uamuzi kuwa liliyotokana na ushahidi wa shahidi wa Nane wa upande wa Mashtaka katika kesi ya msingi, SP Jumanne Malangahe baada ya kuomba mahakama ipokee maelezo aliyoeleza kuwa ni ya mshtakiwa wa tatu (Mohamed Ling'wenya, lakini upande wa utetezi ukayapinga ukitoa sababu tisa.

Jaji Tiganga anarejea sababu hizo za pingamizi la upande wa utetezi dhidi ya upokewaji wa maelezo hayo.

Kutokana na hoja hizo, hoja mbili zilikuwa zinaangalia kifungu cha 27 cha Sheria ya Ushahidi na sababu nyingine zinaangukia kwenye Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Yale ya Sheria ya Ushahidi, ilibidi yashughulikiwe kwa njia ya trial within trial na yale ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai yashughulikiwe kwa kuwasilisha hoja za kisheria mahakamani.

Hivyo baada ya kumaliza usikimizwaji wa kesi ndongo mahakama iliamuru mawakili walete hoja za aina mbili, za majumuisho ya kesi ndogo na za kuunga mkono hoja zinazoangukia kwenye sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai

Jaji Tiganga anarejea mwenendo wa kesi ndogo

Kutokana na haki halisi na wingi wa hoja zilizotolewa mahakama hii haitarejea ushahidi wote kama ulivyotolewa bali kwa kuzingatia hoja inayotakiwa tu kutolewa uamuzi lengo ni kutoufanya uamuzi huu kuwa mrefu

Mtizamo wa kawaida inabidi kuanza kwanza hoja za kisheria, Kisha mambo ya kiushahidi lakini katika shauti hili tumeanza na mambo ya kiushahidi kwa sababu kinacholenga kutolewa ni maelezo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa.

Kwa hiyo tutaanza kusikiliza masuala ya kiushahidi.

Sasa Jaji anaanza kurejea ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ndogo ambao wanalenga kuthibitisha kuwa mshtakiwa huyo alitoa maelezo yake katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Dar es Salaam.

Hivi sasa Jaji Tiganga anarejea ushahidi wa upande wa utetezi akianza na ushahidi wa shahidi wa kwanza wa utetezi ambaye ni mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling'wenya na wa mashahidi wake wawili.

Jaji Tiganga anaendelea kurejea ushahidi wa Ling'wenya na mashahidi wake wengine, huku Ling'wenya mwenyewe akifuatilia kwa makini kuliko washtakiwa wengine ambao wanaonekana kutokuwa na umakini katika kufuatila.Kama ilivyo kwa Ling'wenya ambaye muda wote macho yake yako kwa Jaji Tiganga tu wakati washtakiwa wengine ambao mara nyingi wanaangalia uelekeo tofauti na kwa Jaji.

Jaji Tiganga amemaliza kurejea muhtasari wa ushahidi wa pande zote na sasa anarejea hoja za maandishi zilizowasilishwa na mawakili wa pande zote kuhusiana na Ling'wenya kuwepo au kutokuwepo Dar Polisi kwa tarehe ambayo inadaiwa kuwa ndio maelezo yake yaliandikwa Agosti 7, 2020.

Jaji Tiganga: Ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka yake bila kuacha mashaka na mshtakiwa hapaswi kujionesha kuwa yeye ni mtu mwema bali kuleta mashaka ya maana na kwa sababu hiyo akishaweka mashaka ya maana basi shauri linatakiwa liamuriwe kwa upande wake.

Sasa Jaji anaanza kufanya uchambuzi wa ushahidi wa pande zote kabla yakufikia amri ya hitimisho.

Kielelezo namba 2 cha upande wa Mashtaka (DR) namna kilivyopokewa ni jambo ambalo mahakama hii ilishakitolea uamuzi na Jaji Siyani Oktoba 20, hivyo mahakama inakataa ombi la utetezi kutaka kielelezo hicho kiangaliwe namna kilivyowasilishwa.

Mahakama imepitia ushahidi wa namba mbili wa Mashtaka DC Msemwa na Mahakama imejiuliza kama ni ushahidi ambao unahitaji kuungwa mkono na ushahidi mwingine na vielelezo mbalimbali.

Ushahidi usiohitaji kuungwa mkono uliotolewa bila kiapo.

Ushahidi mwingine kama wa maelezo ya marehemu muda mfupi kabla ya kumsta roho, ushahidi wa mtoto na mwingineo.

Ushahidi wa shahidi wa pili wa Mashtaka si aina ya ushahidi unaohitaji kuungwa mkono.

Lakini pia nimepitia ushahidi wa upande wa Mashtaka basi ushahidi wake umeungwa mkono na ushahidi wa shahidi namba moja ambaye alieleza jinsi alivyomuona na namna alivyoshughulika naye.

Kwa hiyo ushahidi wa shahidi wa pili licha ya kwamba ni aina ya ushahidi usiohitaji kuungwa mkono lakini pia bado umeungwa mkono na shahidi wa kwanza

Hivyo ushahidi wake unakubalialwa moja kwa moja labda kama kutatolewa ushahidi mwingine ambao unajenga mashaka.

Utetezi wamejaribu kujenga mashaka dhidi ya ushahidi huo

Mshtakiwa akidai kuwa alikuwa katika kituo cha Tazara. Hivyo alipaswa kuleta ushahid kuwa alikuwa kituo cha Tazara ingawa kiwango chake cha kuthibitisha hilo.

Mshtakiwa alidai alikuwa Tazara na mshtakiwa wa pili kwa wakati mmoja, hivyo akitakiwa amuite huyo lakini kwa bahati mbaya ingawa huyo mshtakiwa wa pili yuko mahakamani, hakumuita badala yake alimleta shahidi namba tatu ambaye alikuwa Tazara wakati mshtakiwa wa tatu hayupo.

Kwa sababu hiyo ni shahidi namba tatu walikutana tu na mshtakiwa wa tatu ndipo akamweleza kuwa naye alikuwa Tazara

Hivyo ushahidi wa shahidi wa tatu wa utetezi hauna nguvu.

Shahidi wa nne wa mahtaka alikuja na DR ya Tazara ambayo inaonesha katika tarehe hizo mshtakiwa wa tatu hakuwepo Tazara, hivyo mahakama haiwezi kuamini ushahidi wa mshtakiwa wa tatu kuwa alikuwa Tazara.

Shahidi wa tatu wa utetezi alidai kuwa shahidi wa pili wa mashtaka alikuwa Oysterbay Mei 202O na hivyo asingeweza kuwepo Central kwa wakati mmoja.

Hata hivyo vielelezo alivyovileta shahidi wa pili wa utetezi havina uhusiano wowote kwani hakuna mahali ambako vinaonesha kuwepo kwake Polisi Oysterbay, halafu vielelezo vyake vinazungumzia tarehe nyingine.

Ushahidi wake hakuna namna ambayo unaweza kulink na uwepo wa shahidi wa pili wa utetezi Tazara na hivyo thamani ya vielelezo vyake ni ziro haviwezi kuisaidia mahakama.

Pia upande wa mashtaka uliiomba mahamama imuone shahidi huyo kuwa ni shahidi mwenye maslahi na kama ambavyo ilijionesha wakati akiulizwa maswali.

Pia walisema ushahidi wake umejichanganya kwa mfano kuwa na pesa na kumtuma DC Msemwa amnunulie chakula na pengine akasena alipokamatwa hakuwa na pesa yoyote

Pia namna alivyomtambua DC Msemwa, kuwa alimtambua kwa namna mbili, namna alivyomwelezea DC Msemwa kwamba mwanzo alisema DC Msemwa alikuwa mnene, na alipoulizwa tena akakana ushahidi wake wa awali akisema aidha alikuwa mnene kuliko yeye, hivyo wakasema ushahid wake usizingatiwe.

Ingawa mahakama ilishaamua kuwa si kila mkanganyiko unaweza kuathiri ushahidi isipokuwa tu ule unaokwenda kwenye mzizi.

Hata hivyo ushahidi wake ulikuwa unalenga kuthibitisha DC Msemwa alikuwa Oysterbay, kwa hiyo mkanganyiko huo hauwezi kuchukuliwa kwa wepesi.

Hivyo ushahidi wake hauwezi kuzingatiwa.

Lakini pia lazima niseme neno. Ni kweli shahidi huyu ni shahidi mwenye maslahi. Aliulizwa na kueleza anavyofuatilia shauri hili na asivyoridhika na waendesha mashtaka, mashahidi na namna Jaji anavyoendesha kesi hii.

Hivyo huyu ni shahidi mwenye maslahi ambaye ushahidi wake hauwezi kuisaidia mahakama

Hivyo pamoja na kwamba mshtakiwa anapaswa kuleta ushahidi wa kuweka mashaka lakini ushahid wake huo nao haupaswi kuwa wa mashaka.

Kwa sababu hiyo ushahidi wake huo unatulIpiliwa mbali na pingamizi la kwanza kwamba mshtakiwa hakuwahi kuwepo Polisi Central linatupiliwa mbali.

Kuhusu pingamiz kwamba mshtakiwa aliteswa akiwa kituo cha Polisi Mbweni akilazimishwa kusaini maelezo yaliyoandaliwa.

Kama nilivyosema ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa hakuteswa.

Ushahidi wake waliouleta unaonesha walipomfikisha mshtakiwa Mbweni wao waliondoka na walikana kumtesa mshtakiwa akiwa Moshi.

Mshtakiwa anatoa ushahidi kuwa hata baada ya kufikishwa Tazara aliingizwa kwenye chumba ambako alihojiwa na kurekodiwa kwa kamera kisha wakamchukua na kumpeleka kituo Mbweni

Upande wa Mashtaka uliiomba ushahidi wake usikubaliwa wakidai kuwa wakati akitoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa namba mbili hakusema kuwa aliteswa na kwamba hakuweza kuuliza maswali kuhusu kuteswa kwake. Na hivyo ameshindwa kuleta ushahidi kuthibitisha kuteswa

Kimsingi hizo ndo zilikuwa hoja za upande wa Mashtaka.

Upande wa utetezi wameendelea tu kusema kuwa upande wa Mashtaka haujaweza kuleta ushahidi kuthibitisha ikiwemo vielelezo mbalimbali.

Waliikumbusha mahakama umuhimu wa PGO kutaka mshtakiwa kupelekwa kwa daktari anapofokishwa kituoni kwa ajili ya kuthibitisha afya yake na kwamba kama hayo yangekuwa yamefanyika yangeondoa mashaka.

Hivyo waliomba mahakama ione kuwa mshtakiwa aliteswa na maelezo hayo si halali.

Katika hali hiyo pingamizi na ushahidi wa mshtakiwa ambayo 2 unaonesha kuwa shahidi namba 2 na 3 wa Mashtaka walimtisha akiwa kituo cha Polisi Mbweni na kwamba vitisho hivyo ndo vilimfanya akubali kusaini maelezo hayo.

Nimerejea kwa kina ushahidi uliotolewa kwa sababu mbili.

Kwanza mshtakiwa alisema alitolewa Tazara na kupelekwa Mbweni na kwamba alitishwa tarehe 9, Agosti 2020 lakini maelezo ya mawakili yanaonesha kuwa maelezo hayo yaliandikwa tarehe 10, Agosti 2020

Kwa sababu hiyo mahakama inabaki na maswali kuwa mshtakiwa aliteswa au alitishwa au kuteswa lini kwani ushahidi unatofautiana.

Ushahidi kwani wakati wakili anadaia kuwa mshtakiwa alitishwa au aliteswa Agosti 10 mshtakiwa mwenyewe anadai kuwa alitishwa au kutishiwa Agosti 9.

Hivyo hapakuwa na umuhimu kumuita shahidi kutoka Mbweni au suala la mshtakiwa kutakiwa kupelekwa kwa daktari inakosa nguvu maana mahakama bado inabaki kwenye dilemma kuwa ni tarehe ngapi mshtakiwa aliteswa au alitishwa.

Katika mazingira hayo hata pingamizi la pili kuwa mshtakiwa aliteswa au alitishwa linatupoliwa mbali.

Sasa Jaji anaamua hoja za kisheria.

Korti inakubaliana ni kweli mshtakiwa alikamatwa Agosti 5, 2020 na ni nje ya muda wa masaa manne, mshtakiwa anatakiwa kuandika maelezo ya onyo.

Katika hali hiyo Mahakama inasema maelezo hayo yaliandikwa nje ya muda na kukawa na sababu zilizopelelea mtuhumiwa huyo kuchelewa kaandika maelezo ya onyo, basi sababu zinaku alika kupitia kifungu nilichokitaja huku juu.

Kwa mujibu kifungu 50(1) kinatoa kanuni ya jumla kuwa mshtakiwa akikamatwa tu maelezo yake yaandikwe lakini kifungu cha 5(2) kinatoa option kwa mambo kama ya upelelezi wa shauri au muda ambao mshtakiwa anasafirishwa kutoka alikokamtwa kwenda kituo cha Polisi, au mahali popote kwa upelelezi au ugumu wa shauri katika upelelezi muda huo unaondolewa.


Yametolewa maelezo hapa kuwa baada ya washtakiwa kukamatwa kulikuwa na Moses Lujenga ambaye walikuwa na taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba watuhumiwa walikuwa watatu na kwamba huyo wa tatu ali-dissappear ni wazi wasingekaa na kuli-lux bali kuendelea kumkamata.

Hivyo waliendelea kumtafuta

Mahakama inakubaliana na maelezo ya upande wa utetezi kuwa yanaweza kuleta mashtaka lakini hoja iliyoletwa ya kuiomba Mahakama isiyape uzito maelezo hayo imeletwa kabla ya wakati kwani bado maelezo hayo hayajapokewa.


Maelezo ya onyo yanapaswa yaandikwe mahali jalada la msingi lililofunguliwa na katika mazingira haya shauri hili maelezo yalipaswa yaandikwe Dar es Salaam.

Pia kuwasafirisha washtakiwa ni jambo lingine ambalo linafanya kifungu cha 50 (1) kisitumike.

Hivyo kulingana na maelezo yaliyotolewa hapa na upande wa mashtaka hakuna namna ambayo Mahakama hii itaacha kufuata maelekezo ya Mahakama ya Rufani. Kwa hiyo pingamizi la tatu nalo linatupiliwa mbali.


Pingamizi la nne Kutokuandika Sheria kwa usahihi:

Jaji Tiganga: Kwa kuzingatia maelezo ambayo nilishayatoa katika shauri hilo Novemba 9, 2021, Mahakama hii inaona kwamba pingamizi hilo pia halina msingi.

Hivyo mahakama inaona kwamba maelezo ambayo yanataka kutolewa yanaweza kupokewa kwa kuzingatia kwamba hakuna ushahidi uliotolewa wa namna gani ku-cite sheria kimakosa kumemuathiri vipi mshtakiwa.

Hivyo Mahakama inaona hili nalo halina msingi na inalitupilia mbali



Pingamizi la 5: kutokuwepo kwa onyo kutokana na ku-cite sheria sahihi.

Nimeeleza kwa kina na kwa kuzingatia maamuzi ya Mahakama ya Rufani kuwa ku-cite sheria isivyosahihi hakuathiri documents. Hivyo pingamizi hilo nalo linatupiliwa mbali.

Lakini nimeelezewa kuzingatia PGO na katika Maandiko Matakatifu, katika Kitabu cha Yohana 7:51 kuwa hata Mungu mwenyewe hahukumu bila kumsikilza mtu.

Mahakama inaona vitu vyote hivi vinaeleza kuwa mtu asihukumiwe bila kusikilizwa na kwa upekee kuelezwa kosa lake.

Katika kifungu (50) (1) kinachotakiwa ni kwamba mtu aelezwe kosa lake.

Lakini kama nilivyosema katika uamuzi wa Mahakama ya Rufani kuwa kutokutaja kifungu kwa usahihi hakuathiri shahidi pale ambapo hakuna ushahidi wa athari kwa mhusika.

Kwa sababu hiyo Mahakama hii inatupilia mbali hoja hiyo ya tano na inakwenda sasa hoja ya sita ambayo nayo inataka kufanana na hii


Hoja ya sita: Kwamba maelezo yanayoombwa kupokewa hayana kifungu kidogo cha 2 katika kifungu cha 24 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Hoja hii haitaichukulia Mahakama hii muda mrefu. Kwa mujibu wa vifungu 241 na 249 mshtakiwa anatakiwa asomewe substance ya ushahidi.

Ushahidi kama umetolewa chini ya kifungu kilichonukuliwa isivyosahihi, siyi fatal (hakuathiri) ushajidi kwa maana ya substance. Hivyo Mahakama inaona pia hoja hiyo nayo haina mashiko na inalitupilia mbali.

Hoja ya 7: Mshtakiwa anayeanza kukiri maelezo yake kuanza kuandika upya kwamba sasa anakiri.

Upande wa utetezi hawakuizungumzia hivyo mahakama imepata benefit ya maelezo ya upande wa mashtaka.

Pamoja na kwamba upande wa utetezi haujaizungumzia lakini nimeona kweli maelezo haya yanaonekana yameandikwa chini ya kifungu 57 na 58 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Kwa msimamo wa kisheria kinachotakiwa ni format na so kifungu kipi kimetumika. Vifungu hivyo vinaelekeza tu kuwa chini ya kifungu Fulani maelezo yanatakiwa yachukuliwe kwa utaratibu fulani.

Hivyo katika mazingira hayo Mahakama inaona kuwa hoja hiyo ya saba nayo haina mashiko na inalitupilia mbali.

Kwa sababu hiyo hoja zote za pingamizi la utetezi zimetupwa na kwa hiyo mahamama inaona kwamba caustion statement ya mshtakiwa wa tatu ya tarehe 7, 8, 2020 imechukuliwa kwa utaratibu na inatupilia mbali mapingamizi yote na maelezo haya yanapokewa.

Jaji Tiganga: Upande wa mashtaka

Wakili: Mheshimiwa Jaji baada ya uamuzi huo wa shauri dogo tunaomba sasa Mahakama itoe amri ya kurejea kwenye shauri la msingi.

Wakili Kibatala: Msheshimiwa Jaji hatuna pingamizi na amri ya kurejea kwenye shauri la msingi ila tu tunaomba turejeshwe kielelezo aina ya dispatch.

Jaji Tiganga: Na vingine?

Kibatala: Vingine vinabaki kama vilivyo

Jaji Tiganga anarekodi Mwenendo huo kwa muda

Jaji Tiganga: Nimepokea hoja ya upande wa utetezi kuhusiana na kielelezo, ninatoa amri vielelezo vyote vilivyotolewa kwenye shauri dogo virudishwe lakini naelekeza vitolewe copy na ziwe certified.

Jaji: Baada ya uamuzi huu sasa natoa amri ya kurudi kwenye shauri la msingi. Tulipoishia ni ubishi wa kupokewa maelezo haya. Na Sasa Mahakama inaamuru kuwa maelezo haya yanapokewa na kuwa kielelezo cha 13 Cha upande wa mashtaka.

Kwa hiyo shahidi anatakiwa kupanda kizimbani kuelendelea