Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwanda cha maziwa Moshi chalia uhaba wa maji

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akipokea moja ya bidhaa inayozalishwa katika Kiwanda cha Kondiki kilichopo Mwika, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Pamoja na changamoto hiyo, amesema  tangu kiwanda hicho kianzishwe mwaka 2005 kwa ajili ya ukusanyaji wa maziwa, usindikaji pamoja na usambazaji maziwa salama  zaidi ya kaya 1,294 zimeweza kunufaika.

Moshi. Kiwanda cha kusindika maziwa cha Kondiki, kilichopo Mwika Kaskazini wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kinakabiliwa na uhaba wa  maji hali ambayo inatishia uzalishaji wa maziwa katika kiwanda hicho nyakati za kiangazi.


Hayo yamesemwa na Meneja wa Kiwanda hicho, Adrian Kimaro wakati akitoa taarifa ya kiwanda hicho ambapo amesema kiwanda hicho kwa siku kina uwezo wa kuzalisha lita 8,000 za maziwa.


"Eneo hili ambalo kiwanda kipo, tunakabiliwa na changamoto ya maji hasa wakati wa kiangazi na imekuwa ni changamoto ambayo ipo kwa miaka yote, sasa kwa uzalishaji wa maziwa bila kuwa na maji ni changamoto kubwa," amesema Kimario


Aidha amesema katika kila lita moja ya maziwa yanayochakatwa katika kiwanda hicho wanatumia wastani wa lita mbili za maji na kwamba endapo wakichemsha maziwa lita 5,000 kwa siku maji yanayohitajika ni wastani wa lita 10,000.


Pamoja na changamoto hiyo, amesema  tangu kiwanda hicho kianzishwe mwaka 2005 kwa ajili ya ukusanyaji wa maziwa, usindikaji pamoja na usambazaji maziwa salama  zaidi ya kaya 1,294 zimeweza kunufaika  na kiwanda hicho.


"Sasahivi kiwanda hiki kinasindika lita za maziwa 8,000 kwa siku hivyo tunahitaji kukusanya lita 3,000 za ziada ili kufikia uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hiki, na hapa kiwandani maziwa yanayokusanywa kwa wafugaji kila siku husindikwa yote na kuzalisha maziwa mtindi, fresh,  samli, siagi pamoja na yoghat,"


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu  amewaondoa hofu na kusema tayari Serikali imetoa fedha Sh400 milioni  kwa ajili ya maboresho ya vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.


"Serikali tayari imetoa Sh400 milioni kwa ajili ya kuboresha vyanzo vya maji na lengo ni kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyika katika maeneo haya pamoja na kuhakikisha pia wananchi wa maeneo haya wanapata maji ya uhakika," amesema RC Babu