Kiwanda kinaungua moto Dar

Kiwanda cha Jambo ii cha utengenezaji wa bidhaa za plastiki  kilichopo eneo la Vingunguti likiteketea kwa moto

Dar es Salaam. Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umeendelea kuteketeza kiwanda Jambo II cha utengezaji wa bidhaa za plastiki.

Kiwanda hicho kilichopo eneo la Vingunguti, Dar es Salaam kinaendelea kuungua licha ya juhudi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa kuudhibiti moto huo.

Mpaka sasa kwa hali inavyoonekana moto unazidi kusambaa kwa kasi, huku mitambo ndani ya kiwanda hicho zikiendelea kuteketea.

Mpaka sasa ni takriban magari manne ya Jeshi la Zimamoto yapo eneo la tukio yakijaribu kuudhibiti moto huo.

Mpaka sasa upande mmoja wa ghorofa wa kiwanda hicho kimebomolewa.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.


Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi.