Kuigeuza sekta isiyo rasmi kuwa ya kidigitali

Kuigeuza sekta isiyo rasmi kuwa ya kidigitali

Muktasari:

  • Jitihada zake za kutuma fedha nyumbani Tanzania ziliweka msingi wa kutafuta suluhisho ambalo tumelianzisha katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita. Katika kipindi hicho, tulihamia katika maeneo mengine kuliko utumaji wa kimataifa wa fedha nyumbani pekee, lakini wazo la kuunganisha na huduma ambazo zinahusiana na utumaji fedha kimataifa bado ni imara na lenye mashiko.

SWALI:  Kwanza, kwa kifupi eleza historia ya Wakandi na wazo nyuma ya dira ya digitali na mkakati wake.
JIBU. Wazo la Wakandi lilikuja kutoka kwa muasisi wa kampuni, Seleman Mduda, Mtanzania anayeishi
Norway. Jitihada zake za kutuma fedha nyumbani Tanzania ziliweka msingi wa kutafuta suluhisho ambalo tumelianzisha katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita. Katika kipindi hicho, tulihamia katika maeneo mengine kuliko utumaji wa kimataifa wa fedha nyumbani pekee, lakini wazo la kuunganisha na huduma ambazo zinahusiana na utumaji fedha kimataifa bado ni imara na lenye mashiko.

SWALI:  Pia kwa ufupi na ufasaha elezea nafasi ya kampuni hiyo katika suala la ujumuishwaji wa kifedha barani Afrika kwa mukhtadha wa kwa nini Watanzania hawana budi kutumia huduma za kifedha kuweka akiba, kukopa na kufanya miamala ili kuepuka hatari za kuwa na fedha taslimu.
JIBU:Kwetu, mafanikio ya huduma za fedha katika simu za mkononi yameshaweka msingi imara wa ujumuishwaji wa kifedha. Pia kuna sera na sheria nzuri nchini Tanzania. Tunatumia miundombinu hiyo iliyokwishaanzishwa na mawazo na kutengeneza bidhaa ambazo zinasukuma ubunifu ujumuishwaji wa jamii kifedha kwa ajili ya watumiaji wetu.

Swali: Ujumuishaji jamii kifedha umekuwa ni moja ya habari za mafanikio makubwa kwa Tanzania katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, lakini bado suala la watu wasiokuwa na akaunti benki kuingia kwenye mfumo rasmi wa kifedha linaendelea kuwa changamoto kubwa katika ukuaji na maendeleo. Kwa nini iwe hivyo na nani anatakiwa afanye kazi ya kuondoa tatizo la watu kuwa nje katika safari ya ujumuishwaji kifedha kwenda katika viwango vingine?
JIBU: Kwa kutoa bidhaa na huduma kwa kutumia mafanikio ya sasa, tutasukuma suala hilo mbele zaidi. Kazi tunayofanya katika kuyaingiza katika huduma za kidigitali makundi ya kifedha ambayo si rasmi ni kitu muhimu katika kufanikisha ujumuishwaji wa kifedha.

SWALI: Ni kwa jinsi gani ajenda ya ujumuishaji kitaifa katika masuala ya kifedha unaweza kufanikiwa na ni nini nafasi ya kampuni kama Wakandi inapofikia suala la kusaidia nchi kufikia ndoto yake ya kidigitali na ustawi wa jamii kwa kutumia uhamishaji wa teknolojia?
JIBU: Tumekutana na benki nyingi, kampuni zinazoendesha huduma za simu za mkononi (MNO) na serikali katika mikutano tofauti. Picha niliyoiona ni kwamba kila mtu anatafuta njia za kusukuma matumizi ya huduma za kifedha. Mpango wetu ni kuchangia katika kuufanya uchumi uwe wa kidigitali, ambayo haimaanishi ni kufungua akaunti za benki pekee, bali pia kutoa bidhaa na huduma ambazo zina maana kwa watumiaji. Mfano mmoja ni jinsi gani watumiaji ambao wana mikopo SACCOs au kampuni za mikopo midogo wanaweza kulipa mikopo yao kwa njia ambazo hazina ugumu, za haraka na rahisi.

SWALI: Uwekezaji kama wa kuweka mtaji ambao Wakandi inailenga Tanzania ni muhimu na sahihi katika kukuza uhusiano baina ya nchi na nchi?
JIBU: Ubunifu na maendeleo hugharimu. Kwetu, sehemu fulani tunapewa fedha na serikali ya Norway kwa kupitia benki ya maendeleo na ubunifu ya Norway. Hii inaturahisishia kuwekeza katika soko la ndani na kuhakikisha tunachotoa kinaweza kuongeza thamani kadiri iwezekanavyo kwa watumiaji wa mifumo yetu. Wakati huohuo, uwekezaji unazaa ajira Tanzania, na kwa kampuni nyingi, ni vigumu kufanikiwa katika kipindi cha kwanza wakati mapato bado ni madogo lakini yanakua. Kwa minajili hiyo, uwekezaji wa mtaji, kama Wakandi wafanyavyo, unawezesha kufanya kazi ya kuanzisha kwa kipindi kirefu zaidi kulinganisha na kampuni nyingine zinazohitaji mapato kila siku.

SWALI: Watanzania wanatakiwa wategemee nini kutoka kampuni yeni wakati itakapofungua rasmi ofisi hapa na ni jinsi gani uchumi wa taifa utanufaika katika uwekezaji wenu?
JIBU:Wakandi Tanzania LTD tayari ni kampuni iliyoanzishwa Tanzania ambayo kwa sasa inakamilisha kazi inayotakiwa kupata leseni inayohitajika kuendesha shughuli zake nchini. Wakati taratibu zote zitakapokamilika na kuwa rasmi, tumepanga kuwa sehemu muhimu katika soko la ndani kwa ajili ya kampuni changa ili kuzisaidia katika masuala ya kifedha pia na kampuni zilizojijenga zaidi ambazo zinahitaji kile tunachoweza kuwapa katika masuala ya ubunifu. Lakini mwishoni mwa siku, tutakuwa vizuri kama tu tutaweza kuunda bidhaa kwa ajili ya watumiaji wa mwisho ambao wanatumia tunachotengeneza. Pili, tunaamini kuwa tunaweza kuwa wasukumaji wa suala la uwazi ambao matokeo yake utaleta mambo mengi mazuri kwa watu wote wa uchumi usio rasmi na serikali.

SWALI: Zungumzia sifa za Wakandi katika kusaidia kusukuma mabadiliko ya kidigitali Tanzania na matokeo ya shughuli zake katika sekta ya malipo ndani ya nchi, mikopo ya kidigitali na biashara kwa njia ya mtandao.
JIBU: Tunapanga kuwa makini katika malipo na kusambaa. Majukwaa yetu yatafanya kazi kutokea Tanzania, yakijengwa kwa teknolojia ya kisasa na yataendesha ujumuishaji wa kifedha katika ngazi tofauti.
SWALI: Wakandi itasaidiaje kukua kwa eneo la biashara huria barani Afrika na kulifanya liwe na manufaa kwa Watanzania?
JIBU kwa muda mrefu hilo limekuwa na mafanikio katika ujumuishaji wa huduma za kifedha. Licha ya mafanikio makubwa katika ujumuishaji, matokeo ya jumla ya suala hilo yanahitaji teknolojia mpya zaidi ambayo inaweza kuwafanya waongee na kuwasiliana kama vile Open API kwa ajili ya utambulisho wa kitaifa ili kuongeza kasi ya taratibu za malipo katika eneo hili na kuruhusu sera za serikali kubadilika ili kuwezesha makubaliano ya Eneo Huru la Biashara  Barani Afrika (AFCTA) kufanya kazi katika eneo hili. Wakandi itaruhusu uunganishaji nafuu kwa kampuni zinazoanza katika majukwaa ya Wakandi kusaidia ujumuishwaji wa kifedha katika ukanda huu.

SWALI: Kwa nini SACCOs nchini Tanzania na makundi mengine ya kifedha yasiyo rasmi yanatakiwa yaanze haraka kufanya kazi kidigitali na ni jinsi gani Wakandi imejiandaa kuhudumia eneo hilo  na kuwezesha vikundi vya kijamii vya kuweka akiba kusimamia vyema fedha zao na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi?
JIBU: Kitu tutakachotoa katika soko kwa ajili ya SACCOs kinaitwa CAMS. Hicho ni kwa ajili ya mfumo wa usimamizi wa vyama vya kukopo (Credit Association Management System). Kitu muhimu katika CAMS ni kwa wote; maadmini wa makundi, ofisi na wanachama wa SACCOs. Tunaifanya hii isiwe na matatizo kwa wanachama kuingia katika huduma ya fedha kwa simu za mkononi ambazo tayari wanazitumia; pili kwa kuzifanya SACCOs kuwa na uwazi. Itakuwa rahisi kwa wanachama na wadau wengine kujua kinachoendelea ndani. Tunafanyia kazi utoaji taarifa unaojiendesha na mambo mengine mengi yanayowezesha wanachama kutumia teknolojia hiyo na kuweka kidigitali uzoefu wa huduma ambazo kundi linatoa kwa wanachama. Hili litawezesha SACCOs kufuata sheria ambazo zinaziendesha.

SWALI: Tuna Mtanzania ambaye ni mmoja wa waasisi wa Wakandi. Je, hilo si faida na sifa ya kuifanya nchi kuwa kitovu cha uendeshaji wa shughuli zake barani Afrika?
JIBU: Moja ya changamoto kubwa ni kutengeneza huduma kwa soko ambalo hulijui. Kuwa na Mtanzania kama mmoja wa waasisi imekuwa ni mchango muhimu katika mafanikio yetu. Tunaangalia fursa nyingi kwa ajili ya kuweka kitovu kwa bara la Afrika; bila shaka Tanzania ina nafasi kubwa katika hili.

SWALI: Swali la mwisho, unakubaliana na wazo kwamba sehemu hii ya dunia, suala la ujumuishwaji wa kifedha halimaanishi kuhusisha watu wasiotumia benki lakini kuhakikisha linahudumia watu ambao huduma za kibenki haziwezekani kwao?
JIBU: ndio, nakubaliana. Ujumuishwaji wa kifedha tayari unaendelea kwa kiwango kikubwa huku matumizi ya huduma za fedha katika simu za mkononi yakiongoza sekta, bila ya kujali kujumuisha katika huduma za benki wale ambao hawatumii benki.